Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MTUMISHI KUMC AJITOSA UENYEKITI TALGWU TAIFA

MTUMISHI KUMC AJITOSA UENYEKITI TALGWU TAIFA


Na Fadhili Abdallah,Kigoma 

MTUMISHI wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji (KUMC) Mkoani Kigoma Stanslaus Ntatiye amejitosa kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa serikali za mitaa (TALGWU) katika uchaguzi mkuu wa Chama hicho unaotarajia kufanyika mwezi Septemba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma Ntatiye alisema kuwa tayari ameshafanikiwa kupita hatua za awali za mchakato wa uchaguzi na kuthibitishwa kuwa na sifa ya kugombea nafasi hiyo na hivyo kutangaza rasmi kugombea.

Ntatiye alisema kuwa amegombea nafasi hiyo akitimiza azma yake ya kuwa sauti ya Wafanyakazi na kusimamia mifumo ya kitaasisi ya Chama hicho kiweze kusimamia maslahi ya wafanyakazi kikamilifu.

Katika azma yake ya kugombea nafasi hiyo Ntatiye alisema kuwa amepanga kusimamia mambo makubwa matano ambayo ni pamoja na kusimamia maslahi ya wafanyakazi na kujenga na kusimamia mifumo ya kitaasisi ya chama hicho.

Sambamba na hilo Mgombea huyo alisema kuwa amejipanga kusimamia nidhamu ya fedha, uwazi na uwajibikaji , uwwkezaji wenye manufaa kwa wanachama na kuimarisha umoja na sauti ya Wafanyakazi.

Mwisho.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3