KENYA YAAGA MASHINDANO WAFCON 2026
Jul 30, 2026
Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanawake zinaendelea nchini Morocco.
Kenya imekuwa timu ya kwanza kuyaaga mashindano hayo baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 mbele ya Senegal.
Kenya imetolewa kwa kufungwa michezo yote miwili ya mwanzo kwani katika mchezo wa kwanza ilichezea kichapo cha 4-0 mbele ya wenyeji Morocco.
Katika mchezo mwingine wa kundi A, Morocco wamewachapa Algeria 1-0 na kufuzu kwa hatua ya robo fainali.
Leo ni michezo miwili ya kundi B ambapo Ivory Coast inakipiga na Afrika Kusini kabla ya Tanzania kushuka dimbani dhidi ya Burkina Faso.