Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KAMISAA WA SENSA AIPONGEZA REA

KAMISAA WA SENSA AIPONGEZA REA

 



Na Matukio DaimaMedia 


Kamisaa wa Sensa ambae pia ni spika mstaafu wa Bunge la Jamuhuribya Muungano wa Tanzania, Anna Makinda,Makinda amewataka wadau wa sekta ya nishati, kuendelea kusambaza miundombinu ya umeme na nishati safi katika maeneo ya vijijini wananchi ili waweze kunufaika na juhudi za serikali za kuboresha maisha yao.


Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea banda la Rea lililopo katika viwanja vya sabasaba kwa lengo la kupata taarifa ya matumizi ya nishati safi ambapo amesema hatua ya kupeleka umeme vijijini ni mafanikio makubwa katika utekelezaji wa kampeni ya Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanapata umeme na nishati safi ya kupikia.


Amesema kuwa, upatikanaji wa umeme vijijini utawezesha matumizi ya teknolojia mbalimbali za nishati safi, huku akiipongeza Rea kwa hatua kubwa ya kuboresha matumizi ya nishati safi .


"Naamini maeneo ya vijijini yanaweza kupokea teknolojia hizo kwa mwitikio mkubwa zaidi kuliko mijini kutokana na mahitaji yaliyopo kwa wengi wao, kwani huku mjini ni rahisi sana kubadilisha ges inapoisha ikilinganishwa na vijijini"



Aidha, amesema anamshukuru Rais Dk. Samia kwa kila hatua anayoifanya hivyo wanajivunia namna anavyowajali wananchi kwa ujumla


Aidha, amebainisha kuwa suala la kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia, ni muhimu kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa urahisi katika maeneo ya vijijini.


Spika huyo mstaafu amesema upatikanaji wa nishati safi ya kupikia utawasaidia wananchi kupunguza changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo kutokana na matumizi ya nishati zisizo salama.


Aidha, alieleza kuwa matumizi ya gesi yana faida nyingi zikiwemo, kuandaa chakula kwa haraka zaidi, kupunguza matumizi ya kuni na mkaa na kulinda mazingira na afya za wananchi.



Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3