Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KIHONGOSI ATAJA SIRI YA CCM KUENDELEA KUANINIWA NA WATANZANIA

KIHONGOSI ATAJA SIRI YA CCM KUENDELEA KUANINIWA NA WATANZANIA

 


TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII

Na Matukio Daima Media 

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimebainisha misingi mikuu inayokifanya chama hicho kuendelea kuaminiwa na kushinda chaguzi kuu za kiserikali nchini Tanzania.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa .


Kuwa siri ya mafanikio ya CCM inajikita katika mambo makuu matatu ambayo ni utekelezaji wa Ilani, mtandao mpana wa wanachama, na weledi katika kuomba kura.

Kihongosi ameeleza kuwa CCM inashinda kwa sababu ina Ilani ya uchaguzi inayotekelezeka kwa vitendo, ikijikita katika kutatua kero za msingi za wananchi kama upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi ikiwemo maji, umeme, barabara, kilimo, elimu na afya.

Alitolea mfano wa miradi mikubwa kama ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Julius Nyerere, na miradi ya umwagiliaji kama ule wa Ruaha Mbuyuni wilayani Kilolo kama kielelezo cha ahadi zinazotekelezwa.


Aidha, alisisitiza kuwa amani na utulivu ndio msingi mkuu unaowezesha maendeleo hayo kuonekana kote nchini.

Akifafanua sababu ya pili, Kihongosi amesema tofauti na vyama vingine, CCM ni chama chenye watu na mtandao mpana hadi ngazi ya mashina.

Katika kuthibitisha mtandao huo, amekagua uhai wa chama katika mashina mbalimbali na kuridhishwa na uimara wa mabalozi na viongozi wa ngazi za chini.

Amesema kuwa nguvu ya chama hicho inatokana na kuwa na wanachama wengi na wakereketwa ambao wako tayari kukilinda na kukisemea chama chao wakati wote, jambo ambalo washindani wao wameshindwa kulifikia.


Amesema siri ya tatu ya ushindi ni utaalamu wa chama katika kuomba ridhaa ya wananchi kwa kutumia rekodi ya utekelezaji wa ahadi.

Kihongosi ameeleza kuwa CCM haitegemei maneno tupu, bali inaomba kura kwa kuonyesha matunda ya kazi iliyofanyika katika sekta za afya, elimu, na miundombinu.

Aliongeza kuwa chama kiko tayari kwa mijadala na hoja, akiwaalika hata wapinzani kujadiliana kuhusu ujenzi wa nchi badala ya kuibomoa.

Katika hatua nyingine, Kihongosi ametoa onyo kali kwa watumishi wa umma wanaozorota katika utekelezaji wa majukumu yao.

Amesema kuwa CCM ina wajibu wa kuisimamia serikali ili kuhakikisha fedha za walipakodi zinaleta matokeo yaliyokusudiwa.

“Kuna watumishi wa umma wanasema chama kinawafuatafuata; waambieni tutawafuata kweli kweli kama hamtekelezi wajibu wenu,” alisisitiza Kihongosi.



Huku mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Daud Yassin akimkaribisha Kihongosi alipongeza ziara hiyo mkoani Iringa kuwa ni ziara yenye tija kubwa na kuwataka wana CCM kuendelea kutembea kifua mbele na kutosita kueleza kazi nzuri iliyofanywa na serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan .


Huku Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi  Taifa(MCC) Salim Asas, amepongeza kwa kiwango kikubwa utendaji kazi wa serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa imefanikiwa kuleta maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali muhimu kwa ustawi wa wananchi.



Asas alitoa pongezi hizo leo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa. Mkutano huo ulihudhuriwa na mamia ya wananchi na kuongozwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi.

Akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi, Asas alisema kuwa serikali ya Rais Samia imeonyesha dhamira ya dhati katika kusukuma mbele maendeleo ya taifa kupitia uwekezaji mkubwa katika sekta za elimu, afya, miundombinu, maji na nishati. Alibainisha kuwa mafanikio hayo yanaonekana wazi katika maeneo mengi nchini ambapo huduma za kijamii zimeendelea kuboreshwa na kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi.


Alisema kuwa kazi kubwa inayofanywa na serikali iliyopo madarakani inapaswa kupongezwa na kila Mtanzania mwenye nia njema na maendeleo ya nchi. 

Aidha, aliwataka wananchi kuendelea kuiunga mkono serikali yao ili iweze kutekeleza kikamilifu mipango na miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi.

“Tunapaswa kutambua juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi maendeleo. Serikali yake imeendelea kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali nchini,” alisema Asas.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3