Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 UZINDUZI WA KITABU CHA FALSAFA YA SHERIA YA MAMA SAMIA (Mama Samia Doctrine of Law)

UZINDUZI WA KITABU CHA FALSAFA YA SHERIA YA MAMA SAMIA (Mama Samia Doctrine of Law)

Matukio Daima, Dar

WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba anatarajia kushiriki uzinduzi wa kitabi cha Falsafa ya Sheria ya Mama Samia (Mama Samia Doctrine of Law) wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na TPBA kitabu hicho ni maalum kilichoandaliwa kwa lengo la kuandika na kuhifadhi historia ya mageuzi makubwa yaliyofanyika nchini chini ya uongozi wa Rasi Dk. Samia Suluhu Hassan kinatarajiwa kuzinduliwa Juni 12, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa TPBA, Ado Novemba inaeleza kwamba kitabu hicho  kimefanyiwa utafiti wa kina kwa kutumia takwimu, nyaraka rasmi na uchambuzi wa kitaalamu kuhusu mageuzi ya sheria, utoaji wa haki, uchumi, uwekezaji, diplomasia, utawala bora, TEHAMA, elimu, afya na maendeleo ya kijamii. 

Aidha, kitabu kinaeleza kwa kinauhusiano wa mageuzi hayo na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 hadi 2050, kikionesha namna sheria, sera na uongozi vinavyoendelea kujenga msingi wa maendeleo ya Tanzania ya baadaye.

"Kabla ya kuchapishwa, kitabu hiki kilifanyiwa uchambuzi wa kitaalamu na Maprofesa, watafiti na wataalamu mbalimbali na ulilenga kuhakiki maudhui, takwimu na mchango wake katika maendeleo ya taifa" alisema Novemba kupitia taarifa yake.

Mbali na Waziri Mkuu, kiongozi mwingine atakayeshiriki ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na mlezi wa TPBA, Hamza Johari.

MWISHO

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3