TANZANIA IPO SALAMA DHIDI YA EBOLA – WIZARA
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WIZARA ya afya imesemaa kuwa hadi sasa hakuna mgonjwa wa Ebola ambaye amepatikana nchini na kwamba mikakati Zaidi na tahadhari ya kuzuia ugonjwa huo kuingia na kuenea nchini zinaendelea kutekelezwa.
Msimamizi wa huduma za dharula wizara ya afya, Dk.Michael Kremeji alisema hayo akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma wakati wa mafunzo kwa watoa huduma za afya mkoa Kigoma ambao wanahusika na utoaji huduma kwenye maeneo wanayoingia wageni pia kutoka kwenye vituo ambaavyo vitashughulika na mgonjwa pindi itakapotokea.
Dk.Kremeji alisema kuwa mafunzo hayo ambayo yanaendeshwa kwa pamoja biana ya wizara ta afya, Shirika la Afya ulimwenguni (WHO), Kituo cha udhibiti na kuzuia magonjwa (US CDC) na madaktari wasio na mipaka (MSF) yanalenga kuwaweka tayari watoa huduma kuchukua hatua pindi anatopokea mgonjwa wa Ebola nchini ambapo watoa huduma 90 wanapatiwa mafunzo hayo .
Kwa upande wake Daktari anayeshughulika na magonjwa ya mlipuko na majanga kutoka Shirika la Madaktari wasio na mipaka (MSF), Dk.Loveness Isojiki alisema kuwa mafunzo yanayotolewa kwa watoa huduma wa afya mkoa Kigoma yanalenga kuwaweka tayari kupokea wagonjwa na kuwa na utayari wa kujilinda ili wasiambukizwe au kuambukiza jamii nyingine.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Mkuu wa mkoa Kigoma,Balozi Simon Sirro alisema kuwa mkoa Kigoma uko salama dhihi ya ugonjwa huo lakini tahadhari zimeendelea kuchukulia ili kila mtu anayeingia nchini anapimwa kuona hana dalili za ugonjwa huo.
Balozi Sirro alisema kuwa katika kipindi cha karibuni walipatikana raia wawili wa DRC wakihisiwa kuwa na maambukizi ambapo walipimwa na kuweka karantini na ikathibitika kuwa hawakuwa na maambukizi.
Mwisho.
.jpeg)


