Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
RUGWA ATOA MAAGIZO  UJENZI   BANDARI YA KIGOMA

RUGWA ATOA MAAGIZO UJENZI BANDARI YA KIGOMA

 


Kaimu Meneja wa bandari za ziwa Tanganyika, John Fundo (katikati) akitoa taarifa kuhusu utendaji wa bandari ya Kigoma kwa Katibu Tawalaa wa mkoa Kigoma,Hassan Rugwa aliyetembelea na kukagua maendeleo ya miradi ya ujenzi katika bandari hiyo


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Katibu Tawala wa mkoa Kigoma,Hassan Rugwa amewataka viongozi wa kampuni ya Shimizu Corporation ltd ya japan inayotekeleza mradi wa ujenzi wa gati la meli za abiria  na eneo la kusubiria abiria katika bandari ya Kigoma kuhakikisha wanatekeleza mradi huo kwa wakati na  kuacha kutoa visingizo ambavyo havina maana yeyote vinavyochelwesha mradi huo.

 

Rugwa alisema hayo alipofanya ziara na kukagua maendeleo ya mradi huo kusema kwamba viongozi wa kampuni  wanapaswa kutoa taarifa kwa uongozi wa serikali mkoani humo mahali ambapo kuna jambo linakwamisha mradi ili  waweze kupata msaadaa kuliko kutoa taarifa ambazo hazina uhalisia.


Rugwa alisemaa kuwa serikali imedhamiria kuona mradi huo unatekelezwa na kumalizika kwa wakati ili kuleta tija katika kutekeleza demokrasi ya uchumi kwa nchi za ukanda wa maziwa makuu, kuboresha usafiri na usafirishaji wa mizifo na abiria kupitia bandari hiyo sambamba na kuongeza mapato ya serikali hivyo kutomalizika kwa mradi huo kunakwamisha malengo ya serikali.


Awali akitoa taarifa Meneja wa bandari za ziwa Tanganyika, John Fundo alisema kuwa maboresho  mkubwa ya mradi wa ujenzi wa gati la meli za abiria na maboresho ya miundo mbinu ya bandari ya Kigoma umeanza ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa serikali wa kuongeza tija kubwa ya utendaji wa bandari hiyo katika kuhudumia mizigo, abiria na kuongeza mapato ya serikali.

Akitoa taarifa kwa Katibu Tawalaa wa mkoa Kigoma,Hassan Rugwa aliyetembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo Fundo alisema kuwa kiasi cha shilingi Bilioni 43.9  zinatarajia kutumika kutekeleza mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) ukitekelezwa na kampuni ya SHIMIZU CORPORATION ya Japan.


Fundo alisema kuwa katika utekelezaji wa mradi huo upo mradi wa ujenzi wa gati la kusimamia meli za abiria, ujenzi wa jengo la kusubiria abiria na ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kuingia bandarini ambapo kwa sasa mradi huo umefikia asilimia 18 ukitarajia kuchukua miezi 24 kukamilika kwake.


Mwisho.






Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3