Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
POLISI WATOA ONYO KWA BODABODA DHIDI YA KUBEBA WAHALIFU

POLISI WATOA ONYO KWA BODABODA DHIDI YA KUBEBA WAHALIFU

Matukio Daima, Morogoro 

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limewatahadharisha maafisa usafirishaji (waendesha pikipiki) dhidi ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo kubeba wahalifu, mali za wizi na kusafirisha dawa za kulevya.

Tahadhari hiyo imetolewa wakati wa kikao cha maafisa usafirishaji wa Manispaa ya Morogoro kilichohudhuriwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Andrew Kantimbo na maafisa mbalimbali  wa Jeshi hilo.

Akizungumza katika kikao hicho,Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Morogoro ACP Samwel Kijanga amewataka waendesha pikipiki kutumia shughuli zao za kila siku kusaidia vyombo vya usalama kubaini viashiria vya uhalifu badala ya kushiriki katika vitendo hivyo.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Andrew Kantimbo amesisitiza umuhimu wa kutoa taarifa sahihi za uhalifu na wahalifu kwa wakati.


Kamanda huyo wa Polisi amesema kuwa waendesha pikipiki ni miongoni mwa makundi yanayokutana na watu wengi zaidi katika jamii hivyo ni rahisi kuwafahamu na kuwafichua wahalifu.

Naye Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro SSP Gabriel Chiguma ameahidi kuboresha upatikanaji wa mafunzo na leseni huku akiendelea kuhimiza utii wa sheria za usalama barabarani.


Kwa upande wao Maafisa usafirishaji wamepongeza ushirikiano wanaoupata kutoka kwa Jeshi la Polisi kupitia Polisi Kata na kuahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa katika kikao hicho.

Mwisho

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3