Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MIZANI MIPYA YAONESHA MWANGA MPYA KWA WAFANYABIASHARA KILOSA

MIZANI MIPYA YAONESHA MWANGA MPYA KWA WAFANYABIASHARA KILOSA

Na Matukio Daima, Morogoro

WAFANYABIASHARA wa Soko la Mbogamboga Feri- Magole wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wameeleza matumaini ya kuimarika kwa biashara zao kufuatia ugawaji wa mizani unaofanywa na Wakala wa Vipimo Tanzania.

Hatua hiyo inakuja sambamba na wito wa kuacha matumizi ya vipimo visivyo rasmi kama makopo, ndoo za plastiki na visado ambavyo vimekuwa vikitajwa kuchangia malalamiko ya udanganyifu katika biashara.

Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Morogoro, Deogratias Hussein, amesema matumizi ya vipimo rasmi ni njia ya kulinda haki za pande zote mbili, wanunuzi na wauzaji, huku akionya kuwa hatua za kisheria zinaendelea kuimarishwa dhidi ya watakaokaidi maelekezo hayo.


Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Wakala wa Vipimo Tanzania, Francis Olwero, amesema taasisi hiyo inaongeza juhudi za utoaji elimu na usimamizi wa sheria ili kuhakikisha biashara zinafanyika kwa uwazi na usawa.

Mwenyekiti wa soko hilo, Mohamed Said, amepongeza msaada wa mizani uliotolewa, akisema unaondoa mianya ya migogoro na kuongeza imani kwa wateja wanaonunua bidhaa sokoni hapo.


Mwisho

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3