Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
EAC YAPOKEA MSAADA WA EURO MILLION 8 KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MILIPUKO.

EAC YAPOKEA MSAADA WA EURO MILLION 8 KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MILIPUKO.

 


Na,Jusline Marco:Arusha

Jumuiya ya Afrika Mashariki imesaini mkataba kwa kupokea Euro Milioni 5 kutoka serikali ya Ujerumani kwaajili ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko ikiwemo Empox pamoja na Euro milioni 3 kwaajili ya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ikiwa ni pamoja na kuimarisha huduma za afya nchini.


Akizungumza wakati akipokea msaada huo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),Balozi Stephen Patrick Mbundi ameishukuru serikali ya Ujerumani kupitia balozi wake nchini Tanzania kwa msaada huo ambao amesema utasaidia katika mapambano dhidi ya magonjwa ya milipuko kama ebola.


Pamoja na msaada huo pia EAC imepokea vifaa maalum kwaajili ya watoa huduma ya afya kwa wahanga wa magonjwa hayo ya milipuko ili kuweza kujikinga na maambulizi, vile vile tayari imeshapeleka magari 10 yenye vifaa tiba kwa ajili ya kuwezesha watu wenye dalili za ugonjwa kupatiwa matibabu na wataalamu maalum watakao kuwepo.

Aidha amezitaja nchi hizo kuwa ni Burundi, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Rwanda, Sudani kusini, Tanzania pamoja na Uganda.

Kwa upande wake  Dkt .Robert Hongo ameishukuru Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na ubalozi wa serikali ya Ujerumani kwa kutoa msaada wa vifaa ambavyo vitaenda kutumika kwa watumishi wa afya ambapo ndiyo wapo mstari wa mbele kwenye utoaji wa huduma za afya kwa wagonjwa ambao wana magonjwa hatari ya kuambukiza ikiwemo ugonjwa wa Ebola.

Amesema uwepo wa vifaa hivyo vitawasaidia watoa huduma hao kujikinga na kuwajengea hamasa ya kutoa huduma kwa wagonjwa bila ya kuwa na wasiwasi ambapo amesema tangu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ulipoanza mwaka 1976 watumishi wengi wa afya walikuwa wakipata magonjwa huku wengine wakipoteza maisha.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3