Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MEDIA BRAIN NA  KAS WAWANOA WANAHABARI IRINGA

MEDIA BRAIN NA KAS WAWANOA WANAHABARI IRINGA

NA BERDINA MAJINGE,MATUKIO DAIMA MEDIA

Kampuni ya Media Brain kwa kushirikiana na Taasisi ya Konrad Adenauer Stiftung (KAS) imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa Iringa kuhusu uandishi wa habari za kidijitali, yakilenga kuwaongezea uwezo wa kuandaa, kuchakata na kusambaza habari kwa haraka huku wakizingatia misingi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika Mkoani Iringa katika Hotel ya Sunset, Manispaa ya Iringa.

Akizungumza leo june 2,2026 wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Media Brain, Jesse Kwayu, amesema maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na mabadiliko ya jamii, hususan vijana ambao wamejikita zaidi katika matumizi ya mitandao ya kijamii, yanawalazimu waandishi wa habari kuendana na mabadiliko hayo.

Alieleza kuwa matumizi ya majukwaa ya kidijitali yanatoa fursa kwa waandishi wa habari kuwafikia watu wengi zaidi kwa wakati mfupi, hivyo ni muhimu kwao kuongeza ujuzi wa kutumia teknolojia hizo kwa ufanisi bila kuathiri ubora na uaminifu wa habari wanazozitoa.

Washiriki wa mafunzo hayo walipata fursa ya kujifunza mbinu mbalimbali za uandishi wa habari za kidijitali, matumizi ya mitandao ya kijamii katika utoaji wa habari, pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto zinazoibuka katika mazingira ya habari ya kisasa.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3