Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MABORESHO UWANJA WA NDEGE KIGOMA KUKAMILIKA OKTOBA

MABORESHO UWANJA WA NDEGE KIGOMA KUKAMILIKA OKTOBA

                            

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WAZIRI wa uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa uwanja wa ndege wa Kigoma utaanza kutoa huduma mwezi November mwaka huu baada ya ukarabati na maboresho makubwa ya uwanja huo kukamilika.

Waziri Mbarawa alisema hayo alipofanya ziara kutembelea na kukagua uwanja huo jana alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuboresha miundo mbinu ya usafiri na usafirishaji kwa mkoa Kigoma.

Alisema kuwa maboresho ya uwanja huo ni sehemu ya kuboresha miundo mbinu ya mkoa Kigoma ambao serikali umeuteua kuwa mkoa Kimkakati kwa mambo ya uchumi na biashara kwa ajili ya soko la Maziwa Makuu hivyo serikali inasimamia maboresho hayo kuhakikisha uwanja unakamilika na kuanza kufanya kazi ili kutekeleza mpango huo kwa ufanisi.

Profesa Mbarawa alisema kuwa uwanja huo unatarajia kuchukua ndege kubwa ikiwemo Boing 737 lakini pia uwanja utawekwa taa hivyo kuweza kufanya kazi kwa saa 24 kuruhusu ndege kutua wakati wote na kwamba kandarasi wa uwanja huo , China Railway Construction Engineering amewahakikishia kuwa uwanja utakamilika mwezi julai mwaka huu.

Akitoa maelezo kwa Waziri Mbarawa kuhusu utekelezaji wa mradi huo Mkuu wa viwanja vya ndege kanda ya Magharibi, Mhandisi  Fadhili Magenema alisema kuwa kwa sasa mradi huo umefikia asilimia 60 ukitarajia kukamilika mwisho wa mwezi julai mwaka huu ambapo vifaa mbalimbali vitaanza kufungwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba ili uanze kutumika Novemba mwaka huu.

Mhandisi Magenema alisema kuwa maboresho hayo yanahusisha maeneo manne ambayo ni jengo la abiria, upanuzi wa njia ya kuruka ndege, sehemu ya mnara wa kuongozea ndege na sehemu ya maegesho ya magari mradi ukitarajia kugharimu shilingi Bilioni 51 na uwanja unaweza kuhudumia abiria 500 kwa wakati mmoja.

 mwisho.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3