Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KISEZ  KuCHOCHEO DIPLOMASIA YA UCHUMI KIGOMA

KISEZ KuCHOCHEO DIPLOMASIA YA UCHUMI KIGOMA


Na Fadhili Abdallah,Kigoma


Eneo maalum kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na shughuli maalum za kiuchumi na biashara (KISEZ) lililopo Ujiji manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma linaelezwa kuwa kichoocheo kikubwa cha utekelezaji wa Diplomasia ya uchumi kwa nchi za ukanda wa maziwa makuu.

Katibu Tawala wa mkoa Kigoma, Hassan Rugwa alisema hayo alipotembea kiwanda cha vinywaji baridi, sabuni na mafuta ya kula kinachojengwa na raia wa Burundi ambacho kinatarajia kuanza uzalishaji mwezi Oktoba  mwaka huu.

Rugwa alisema kuwa wakati raia huyo wa Burundi akiendelea na ujenzi wa kiwanda hicho pia yapo maombo ya raia weengine wa Burundi na jamhuri ya kidemokrasi ya Congo (DRC) ambao wameomba maeneo kwa ajiili ya ujenzi wa viwanda na shughuli za kiuchumi ambapo KISEZ kwa sasa lina eneo la ukubwa wa Hekari 16,000 ambazo zimetengwa kwa shughuli hiyo.

Katibu Tawala huyo wa mkoa Kigoma aliwakaribisha wawekezaji Zaidi kujitokeza kuwekeza katika eneo hilo ambapo alisema kuwa wawekezaji kutoka nje wanachangia uwepo wa uhakika wa masoko hapa nchini na kwenye nchi wanazotoka hivyo kupanua Zaidi shughuli za kiuchumi na biashara za kimataifa.

Awali Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Nmugizi Appolinari alisema kuwa wanatarajia kuwekeza kiasi cha Shilingi bilioni 2.5 katika kiwanda hicho wakitarajia kuzalisha vinywaji baridi ikiwemo soda, juice, mafuta ya kula, sabuni za kufulia na kuogea.

Apolinari alisema kuwa mazingira salama ya mkoa na uhakika wa masoko kwa Burundi na Tanzania ndiyo yaliyomvutia kuwekeza mkoani Kigoma na kwamba majengo ya kiwand yanatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi julai na mitambo ya kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kiwanda hicho itaanza kufungwa mwanzo mwa mwezi Agosti kwani tayari mitambo hiyo imeshawasili bandari ya Dar es Salaam.

Mwisho.



 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3