AGRI TERRA NA IFCU WAANZA KUWAKOMBOA WAKULIMA WA UFUTA IRINGA
Wakulima wa zao la Ufuta wakivuna zao hilo
Na Francis Godwin ,Matukio Daima Media
CHAMA Kikuu cha Ushirika mkoani Irin-ga, (IFCU) kwa kus-hirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Agri Terra wamewapeleka wakulima wa ufuta 25 mkoani Mtwara kwa ziara ya mafunzo, ili kujifunza kilimo bora na matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani.
Akizungumza na wakuli-ma hao, Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika, Tumaini Lupola, amesema kuwa zi-ara hiyo IFCU imeshirikiana na shirika Agri terra la nchini Uholanzi linaloshughulika na vyama vya ushirika hasa katika kuvijengea uwezo vya vya ush-irika kwenye masuala ya ush-awishi lengo likiwa kuwasaidia wakulima kubadilishana uzoe fu na wakulima wa Mtwara ku-husu zao la ufuta.
ziara ya "Tunafanya wiki moja na wakulima wetu wanaolima ufuta kutoka mae-neo mbalimbali ya mkoa wa Iringa, hasa katika Wilaya ya Iringa na Wilaya ya Kilolo. Lengo kuu la ziara yetu hii ni kwenda kujifunza kwa wenzetu wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mtwara na Tumeanzisha mfumo wa stakabadhi ghala-ni lakini uelewa wa wakuli-ma wengi bado ni mdogo, na wengi wanaonekana kuwa na mashaka na mfumo huu.
Lakini ukiangalia kwa ma-kini, wakulima wa kule Mtwara wanaotumia mfumo huu wamepata mafanikio makub-wa ukilinganisha na kipindi cha nyuma. Tunategemea baadhi ya wawakilishi wanaokwenda huko, watarudi na matokeo chanya ambayo yataondoa wasiwasi wa wakulima wa huku"
Aidha kwa upande wao wakulima wa ufuta mkoani Iringa wameeleza matarajio yao ya kujifunza kutoka kwa wakulima wenzao mbinu bora za kilimo cha ufuta na namna wanavyonufaika na mfumo wa stakabadhi ghalani.
Akizungumza na Matukio Daima Media , mmoja wa wakuli-ma wa zao la ufuta, Hezdon Chusi kutoka Wilaya ya Kilo-lo, amesema kuwa anatarajia mafunzo hayo yatamsaidia kuwa mkulima bora wa ufuta.
"Matarajio yangu ya safa-ri hii ni kwenda kujifunza kwa wakulima wenzangu namna wanavyolima ufuta, wanavy-otunza, na jinsi walivyounda vyama vya ushirika.
Lengo langu ni kurudi na kufanya kama wanavyofanya wenzetu, ikiwa ni pamoja na uzalishaji bora wa zao la ufuta.
Pia kuwepo kwa soko zuri kupitia ushirika kutasaidia uki-angalia kwa sasa, wakulima wengi tunalima kiholela na ndiyo maana faida imekuwa ndogo Lakini safari hii naamini itatuletea mafanikio zaidi,"
Naye Silus Kalinga, mkuli-ma wa ufuta kutoka Usolanga, ameeleza jinsi mfumo wa stak-abadhi ghalani ulivyoongeza thamani ya soko la zao hilo, ukilinganisha na kipindi cha nyuma walipokuwa wakitege mea walanguzi.
"Awali tumekuwa tukiuza ufuta wetu kupitia walanguzi waliokuwa wakipima mazao yetu kwa njia isiyo sahihi kwa kutumia madebe hii imetunyo nya sana wakulima lakini Tu-nashukuru chama chetu cha ushirika kwa kuleta mfumo wa stakabadhi ghalani unaotumia mizani ya kisasa Hii imekuwa ni neema kubwa kwa wakuli-ma, na naamini italeta changa moto chanya kuongeza uzal-ishaji,"
Kwa upande wake mkuli-ma Agness Malenda kutoka Tarafa ya Idodi amesema kuwa awali walikuwa wakilima zao hilo bila elimu ya kutosha, hivyo anatarajia kupata maari-fa yatakayowawezesha kulima kwa tija.
"Matarajio yangu makub-wa kupitia ziara hii ni kupa-ta elimu itakayotutoa katika kilimo holela ukizingatia hii itakwenda kutuongezea ujuzi na maarifa ambayo tumeanza kuyapata kupitia chama cha ushirika ili tuanze kulima kwa faida na kwa taarifa tulizope-wa, wenzetu wanalima kwa elimu na faida yao ni kubwa tuna imani kubwa ya kwenda kuanza kilimo chenye ubora,"
Aidha wakulima hao wa-metoa pongezi kwa Chama cha Ushirika kwa kuwajen-gea uwezo na kuwapa elimu itakayowawezesha kulima kili-mo cha faida na chenye tija.
