Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WAZIRI NDEJEMBI- AWASILI NGARA KAGERA KWA ZIARA YA KIKAZI

WAZIRI NDEJEMBI- AWASILI NGARA KAGERA KWA ZIARA YA KIKAZI


Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius J. Ndejembi amewasili wilayani Ngara mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Kanali Martius Kahabi


Amepewa mapokezi pia na viongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera, wakiwemo Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Stephen Mashauri Ndaki, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ngara, Vitalis Ndailagije pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Dotto Bahemu.

Akiwa wilayani Ngara, Waziri Ndejembi ataweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Benaco hadi Kyaka pamoja na kituo cha kupoza umeme cha Benaco.

Katika ziara hiyo, Waziri Ndejembi ameambatana na Kamishna Msaidizi wa Umeme Wizara ya Nishati, Mhandisi Christopher Bitesigirwe, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO.


 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3