WAZIRI DKT GWAJIMA AWAWEZESHA VYEREHANI WAHITIMU WOTE WA USHONAJI CHUO CHA RUNGEMBA
NA MATUKIO DAIMA MEDIA ,MUFINDI
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba wilayani Mufindi mkoani Iringa, Kidubya Kulamiwa, amesema Serikali imeweza kuwatunuku wahitimu wa mafunzo ya ushonaji vyerehani ambavyo vitawasaidia kupunguza changamoto ya ajira na kuwawezesha kuanzisha maisha mara baada ya kuhitimu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kidubya amesema jumla ya wahitimu takribani 40 wamehitimu katika mafunzo hayo ya ushonaji ambapo pia walipatiwa vyeti pamoja na vyerehani vya kuanzia shughuli zao.
Alisema chuo hicho kilipokea msaada wa vyerehani kutoka Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum chini ya waziri Dkt Doroth Gwajima , ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha vijana kujitegemea kiuchumi.
“Sisi kama chuo tulipokea vyerehani kutoka serikalini kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kama sehemu ya kuwawezesha kujitegemea kiuchumi ambapo wahitimu wa awali walikuwa 30 na leo ni kundi la pili ambalo lina wahitimu 40,” amesema Kidubya .
Ameongeza kuwa mafunzo hayo yamejikita zaidi katika vitendo, hususan ushonaji na matumizi ya mashine.
“Walichojifunza hasa ni ushonaji kwa maana ya namna ya kutumia mashine za ushonaji na namna ya kubuni (design) nguo mbalimbali pamoja na ushonaji wenyewe.
Aidha, amesema Serikali iliona umuhimu wa kuwasaidia wahitimu hao ili wasirudi mtaani bila mtaji.
“Mara baada ya kuhitimu Serikali iliona kwamba wasirudi mtaani kuanza kuhangaika pa kuanzia, ndiyo maana imetoa vyerehani katika makundi, ambapo vyerehani takribani 10 vimetolewa kwa makundi ya watu wanne wanne, ili waweze kuvitumia kuanza shughuli za ushonaji na kujipatia kipato cha kila siku,
Hata hivyo Kulamiwa alielezea programu ambazo zinapatikani katika Chuo hicho zikiwa na lengo la kusaidia Vijana na Jamii ili kuweza kujikwamua katika changamoto ya ukosefu wa Ajira na utegemezi.
"Programu hii kama nilivyosema hapo awali inalengo la kuwainua wananchi waweza kujitegemea kuwapa maarifa sio Kwa nadharia Bali Kwa vitendo ili waweze kujitegemea sambamba na hilo pia chuo inazoprogram nyingine zinazotoa mafunzo Kwa Jamii ,mafunzo ya Kompyuta pia uokaji wa vitafunwa mbalimbali.
Pia aliongeza kuwa kama Chuo wamelenga kutoa huduma Kwa wananchi na hili linathibitika Kwa wahitimu hao 40 ambapo Chuo kimeghramia Kwa 100% gharama zao zote za mafunzo ili kuweza kuisaidia serikali kutimiza ahadi yake kufuatia maagizo yaliyotolea na Rais Dkt. Samia Suluhu ya kutuma Vyuo vyote vya Ufundi kuweza kuwa na kozi za kusaidia Jamii pamoja na Vijana ili kuondoki na changamoto.
Aidha amewaomba wanachi kuweza kujitokeza Kwa wingi katika chuo hicho ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali Ambayo yatasaidia maendeleo ya Jamii.
pia alitoa pongezi zake Kwa serikali ya awamu ya sita Kwa kuwawezesha kuboresha Hali ya Vyuo vya Ufundi ambavyo Kwa kipindi Cha nyuma havikuwa na hali nzuri lakini kupitia msaada wa serikali maboresho mengi yamefanyika ambayo yanachochea maendeleo katika Jamii .




.jpeg)



