Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WANANCHI WAPEWA TAHADHARI DHIDI YA MATAPELI WA UWEKEZAJI

WANANCHI WAPEWA TAHADHARI DHIDI YA MATAPELI WA UWEKEZAJI

 Na Samwel Mpogole

Wananchi wametakiwa kuwa makini na matapeli wa uwekezaji ikiwemo wanaotumia mitandao ya kijamii kuwahadaa wananchi kwa ahadi za faida kubwa na zisizo halisi.

Tahadhari hiyo imetolewa na Afisa habari na Uhusiano kwa Umma kutoka Mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana (CMSA) Stella Anastazi katika maonesho ya Biashara ya Mbeya City Expo 2026 wakati wa mahojiano maalumu kuhusu masuala ya uwekezaji na usalama wa fedha za wananchi.

Stella amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakivutiwa na matangazo ya uwekezaji yanayoahidi faida kubwa kwa muda mfupi bila kufanya uhakiki wa kampuni husika.

"Ni muhimu wananchi kuhakikisha uhalali wa taarifa za uwekezaji wanazozipokea kwa kuwasiliana na Mamlaka husika ili waweze kuwekeza katika taasisi au kampuni ambazo zimeidhinishwa na kupatiwa leseni   na hivyo kuepuka kutapeliwa na  kupoteza fedha zao," amesema Stella.

Aidha amesema CMSA inaendelea kutoa elimu kwa wananchi hususani vijana kuhusu umuhimu wa uwekezaji salama, matumizi sahihi ya fedha pamoja na umuhimu wa kuanza kuwekeza mapema.

Amesema masoko ya mitaji yanatoa fursa za kukuza uchumi kwa wananchi kupitia bidhaa mbalimbali zinazoendeshwa na kusimamiwa na wataalamu wa masoko ya mitaji.

Baadhi ya wananchi waliofika katika eneo la banda la Taaisisi hiyo kwajili ya kujipatia elimu wamesema elimu ya uwekezaji bado inahitajika zaidi kutokana na kuongezeka kwa matukio ya utapeli mtandaoni.

Mkazi wa Rungwe Mbeya, Daniel Mwakipesile amesema watu wengi huvutiwa na ahadi za faida kubwa bila kuelewa hatari zilizopo.

"Watu wengi wanaingia kwenye uwekezaji kwa haraka wakiamini watapata fedha nyingi, lakini mwisho hupoteza fedha zao," amesema.

CMSA imewataka wananchi kutumia njia rasmi za uwekezaji na kutafuta taarifa sahihi kabla ya kuwekeza fedha zao.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3