WABUNGE WACHANGIA BAJETI YA ELIMU TRILIONI 2.398 DODOMA
May 8, 2026
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaendelea kuchangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2026/2027, iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma.
Bajeti hiyo iliwasilishwa Mei 7, 2026 na Waziri wa Wizara hiyo, Adolf Mkenda, akiomba jumla ya shilingi trilioni 2.398 kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo ya sekta ya elimu nchini.
Katika michango yao leo Mei 8, 2026, wabunge wameelekeza hoja na mapendekezo yanayolenga kuongeza ufanisi, ubora na tija katika utoaji wa elimu, wakisisitiza umuhimu wa fedha hizo kuelekezwa kwenye maeneo yenye mahitaji makubwa ili kuleta matokeo chanya kwa taifa.
