VYAMA VYA SIASA VYAIPONGEZA WIZARA YA KAZI, AJIRA NA MAHUSIANO KUWEKEA MKAZO MAHUSIANO.
Matukio Daima, Morogoro
Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini wanaipongeza Serikali kwa kuunda Wizara ya Kazi, Ajira na Mahusiano, wakisema hatua hiyo inasaidia kujenga mwafaka na uelewa wa pamoja kati ya Serikali na makundi mbalimbali ya kijamii.
Viongozi hao wanasema kupewa uzito kwa suala la mahusiano kunachangia kufanikisha mipango ya maendeleo pamoja na kuimarisha usalama, amani na utulivu wa nchi.
Kauli hizo zinatolewa mjini Morogoro wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Juma Ali Khatibu, anasema mabadiliko hayo yanaonesha dhamira ya Serikali ya kuimarisha maelewano na ushirikiano kati ya wadau wa maendeleo.
Katibu Mkuu wa CHAUMA, Salum Mwalimu, anasema dhana ya mahusiano inaweza kusaidia kujenga mazingira bora ya majadiliano na kupunguza migogoro.
Naibu Katibu Mkuu wa SAU, Asha Juma, anasema ushirikiano kati ya Serikali na vyama vya siasa ni msingi wa maendeleo ya kidemokrasia.
Mwenyekiti wa TLP, Richard Lyimo, anasema hatua hiyo inaongeza mshikamano wa kitaifa.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, anasema lengo la kikao hicho ni kujenga uelewa wa pamoja kuhusu mabadiliko ya kimuundo serikalini.
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Zuhura Yunus, anasema kuongezwa kwa kipengele cha mahusiano kunalenga kuimarisha ushirikiano na maelewano kati ya Serikali na wadau mbalimbali.Mwisho

.jpeg)

.jpeg)