TUNAOMBA WANAISIMANI WOTE JUNE 1 KURA ZOTE KWA MTATIFIKOLO-MCC ABOOD
NA BERDINA MAJINGE,
MATUKIO DAIMA MEDIA.
IRINGA.Wananchi wa jimbo la Isimani wameobwa kujitokeza kwa wingi kumpigia kura za ndio Mgombea ubunge wa jimbo la Isimani Emmanuela Mtatifikolo ili kubeba mikoba ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Marehemu William Lukuvi.
Ombi hilo limetolewa na Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa na mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa Mohamed Aboud wakati wa uzinduzi wa kampeni Chama cha Mapinduzi Jimbo la Isimani na kuwataka wana Isimani kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura June 1,2026 wasiishie kusema chama kimeshinda au Emmanuela kashinda wakati hawajapiga kura.
Alisema kuwa kamati ilikaa na kujua kuwa Emmanuela atavaa viatu vya Lukuvi na kwamba mgombea huyo amejipanga kushughulikia changamoto zote za wana isimani.
"Niwahakikishie baada ya kumchagua Emmanuela ndani ya miezi sita mtaona matokeo ya juhudi zake na utendaji kazi wake na mtaamini kuwa viatu vya Lukuvi vimemtosha sawa sawa" alisema
Alisema kuwa moja ya mambo amabayo anatakiwa kuyaendeleza ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Pawaga hadi Iringa mjini,skimu ya umwagiliaji pamoja na kilimo na ufugaji sambamba na yale yote ambayo Marehemu Lukuvi aliyaanza na kuyaacha bila kukamilika.
Wakizungumza wabunge wa Mkoa wa Iringa wakati wakimuombea kura Mgombea Emmanuela Mtatifikolo walisema kuwa mgombea huyo ni mtiifu na mchapakazi na msikivu na kuwaomba wana Isimani kumpigia kura za ndio ili aweze kuwa mbunge wao na kwenda kutekeleza yale yote yaliyoachwa na Lukuvi.
Kwa Upande wake Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Emmanuela Mtatifikolo alisema kuwa amepokea mikoba ya Lukuvi akiamini kuwa anaweza kutenda zaidi ya alivyofanya marehemu Lukuvi.
Alisema kuwa aliamua kwenda kugombea katika jimbo hilo baada ya Kifo cha Lukuvi watu wengi walipata wasiwasi na kujiuliza itakuwaje ndipo akaamua kurudi nyumbani kugombea ili kuwatoa wasiwasi wana Isimani.
" Wakati wa kifo cha Marehemu Mh Lukuvi wananchi wengi walikuwa na majonzi na huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao wakati huo wanajiuliza itakuwaje nani atabeba mikoba,ndipo nikaamua kuja kugombea kwa sababu nina uwezo wa kukabiliana na changamoto za jimbo hili"
“mimi sina maneno mengi napenda matokeo zaidi hivyo naomba mnichague kwa kura nyingi ili niwatoe wasiwasi wa maendeleo katika jimbo hili”alisema
Mtatifikolo aliongeza kuwa anaishukuru serikali ya CCM chini ya uongozi wa Lukuvi kwa kuliongoza jimbo la Isimani kwa miaka 30 imefanya kazi kwa bidii na kuleta maendeleo katika jimbo hilo.
Akizungumzia maendeleo yaliyopatikana katika upande wa afya alisema kuwa awali wananchi walikuwa wanafariki kwa kukosa maji mwilini jambo ambalo Lukuvi alitatua kwa kupeleka huduma za afya,zahanati na vituo vya afya ambavyo vinaendelea kujengwa.
“Serikaliya awamu ya sita imeleta miradi mingi ya maendeleo ikiwemo afya, maji, uchumi pamoja na miundo mbinu ya barabara”
Akizungumzia suala la uchumi Mtatifikolo alisema kuwa atahakikisha wana pawaga wananufaika na zao la mpunga kwa kulisha nchi pamoja na nchi za jirani kwa kuwatafutia soko la uhakika.
Katika upande wa barabara alisema atahakikisha barabara ya Isimani Izazi, inajengwa kwa kiwango cha lami sambamba na barabara ya pawaga Iringa mjini ambao tayari Mbunge wa Iringa mjini Fadhili Ngajilo na Lukuvi waliisha iombea fedjha za ujenzi ikiwa pamoja na kukamilika kwa wakati.
“Nimekabidhiwa mikoba ya Lukuvi hivyo nimejipima na kuona natosha sana kuweza kutimiza yale yote ambayo alitamani wana Isimani wayapate,sambamba na kutekelza ilani ya chama, lakini haya yote hayawezi kufanikiwa kama hamtapiga kura june 1,2026”alisema
Akizungumza MCC Salim Abri alisema kuwa anamfahamu Emmanuela kwa utendaji kazi wake kupitia miradi mikubwa ya serikali ambayo imefanikiwa zaidi hivyo anaimani kubwa na uongozi wake.
“Kwa hiyo kama wanaisimani wakisema wanashida ya maji au afya Emmanuela atakuwa anafahamu zaidi kwa sababu ni mtoto wa kijijini anafahamu zaidi wanaisimani wanataka nini”alisema
MWISHO.
.jpeg)
.jpeg)


