SIRRO ATAKA VIKWAZO BIASHARA ZA KUVUKA MPAKA VIONDOLEWE
Na Fadhili Abdallah,Bujumbura
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amezitaka mamlaka za kibiashara za Tanzania na Burundi kushughulikia changamoto ya vikwazo visivyo vya kikodi ili kuimarisha Biashara baina ya mataifa hayo mawili.
Balozi Sirro ametoa wito huo akizungumza katika ufunguzi wa wa maonesho ya pamoja ya biashara baina ya Tanzania na Burundi yanayofanyika jijini Bujumbura nchini Burundi yakijumuisha wajasiliamali na wafanyabiashara kutoka mkoani Kigoma na wale wa Burundi.
Akimwakilisha Waziri wa viwanda na Bishara kufungua maonyesho hayo Mkuu huyo wa mkoa Kigoma alisemaa kuwa pande hizo mbili zina nafasi ya kushughulikia na kuondoa changamoto hizo zisizo za kikodi kurahisisha ukuaji wa biashara.
Mkuu huyo wa mkoa kigoma alisema kuwa Tanzania na Burundi zinapaswa kushughulikia vikwazo hivyo ikiwemo taratibu za zinazochukua muda mrefu , utoaji wa maamuzi ya busara bila kuzingatia kanuni na Sheria pamoja na kuharakisha utekelezaji taratibu za biashara na wafanyabiasha wanaofanya biashara za kuvuka mpaka.
Awali Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Gelasius Byakanwa akizungumza katika maonesho hayo alisema kuwa maonesho hayo yamelenga kutanua wigo wa masoko na kuwezesha wafanyabiashara wapya kuingia kwenye sekta hiyo na biashara zao kuwa zenye tija.Kwa upande wake Josias Bigirimana ambaye ni mfanyabiashara kutoka jiji la Bujumbura nchini Burundi alisema kuwa maonesho hayo ya pamoja, yamewapa fursa ya kubadilishana ujuzi na taarifa za kimasoko baina yao na wafanyabiashara wa Tanzania.
Mwisho.


