RC KHERI AWATAKA WANANCHI IRINGA KUSHIRIKI WIKI YA UTAFITI ,UBUNIFU NA HUDUMA ...
Na Matukio Daima Media
Mkoa wa Iringa unaandaa Maadhimisho ya Wiki ya Utafiti, Ubunifu na Huduma kwa Jamii ambayo yatafanyika tarehe 2 hadi tarehe 4 Juni, 2026 katika Viwanja vya Bustani ya Manispaa ya Iringa.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kheri james amesema kuwa Ili kufanikisha shughuli hiyo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imekiteua Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kuratibu Maadhimisho hayo.
RC Kheri alisema kuwa ufunguzi wa maadhimisho hayo utafanyika siku ya tarehe 2 Juni 2026, katika Viwanja vya Bustani ya Manispaa ya Iringa.
Maadhimisho hayo yamebebwa na kaulimbiu isemayo: "Harnessing Tanzania's Mineral Wealth for Renewable Energy, Digital Transformation and Societal Security" yaani "Kutumia Utajiri wa Madini wa Tanzania katika Kukuza Nishati Jadidifu, Mageuzi ya Kidijitali na Usalama wa Jamii."
Kaulimbiu hiyo inaenda sambamba na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na maono ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kuhimiza matumizi ya sayansi, teknolojia, ubunifu na ushirikiano wa taasisi mbalimbali kama nguzo muhimu za maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.
“Hivyo, tunatoa wito kwa taasisi zote za umma na binafsi, wadau wa maendeleo, sekta binafsi, wabunifu, watafiti na wananchi kwa ujumla kutumia fursa hii adhimu kushiriki kikamilifu katika maonesho haya, kujifunza, kuonesha mafanikio yao, na kujenga ushirikiano utakaosaidia kuijenga Tanzania yenye maendeleo endelevu na ushindani wa kimataifa”alisema
Kheri James aliongeza kuwa maadhimisho hayo yanabeba tija ya maadhimisho hayo ambayo ni ushirikishwaji mkubwa wa wadau kutoka sekta mbalimbali za Serikali na zisizo za serikali;Utoaji wa huduma mbalimbali bure kwa wananchi wote watakaofika kwenye maadhimisho hayo,.
“Kupima afya zao; Kupata ushauri wa masuala mbalimbali ya kisaikolojia na biashara,Upimaji wa usikivu ili kujua kiwango cha usikuvu na kupata ushauri; na Uchangiaji damu wa hiari”alisema.
Aidha Kheri James alitumia wasaa huo kuutangazia umma kuhusu maadhimisho hayo makubwa yanayoleta juhudi za pamoja kwenye Mkoa wa Iringa, na kuwasihi wananchi wote wa Iringa na mikoa ya jirani kushiriki.
“Niwaombe wadau wote muhimu kujitokeza kushiriki kwa kuonesha bidhaa au huduma zao. Ili kushiriki, wasiliana na uongozi wa Chuo cha Mkwawa mapema ili kurahisisha taratibu za maandalizi, na kupewa nafasi, kwa kuwa nafasi ni chache”alisema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa utafiti na ubunifu chuo kishiriki cha elimu Mkwawa Dkt Celina Mkimbili ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wadau katika Maadhimisho ya Wiki ya Utafiti, Ubunifu na Huduma kwa Jamii.
Mkimbila ameeleza kuwa watakuwa na tafiti mbalimbali ambapo wametafiki miradi 25 ambayo itaonyeshwa ikiwemo utafiti juu ya zao la ulanzi na uyoga.
“Wamegundua ulanzi unaweza kuleta mazao mbalimbali ambayo yananatatua matatizo mbalimbali ya jamii mfano spiriti,na bethano hivyo tunagegemea kuwa na wawekezaji na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi wanaofanya biashara ya ulanzi ili wafanye mashirikiano na watafiti wa mkwawa”alisema.
Aidha amesema kuwa utafaiti wa uyoga unafanyika katika chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa watafiti wamegundua namna ambavyo wananchi wanaweza kulima uyoga zao ambalo litaleta afya kwa watumiaji na kutumika kwa namna mbalimbali.
Alisema kuwa uyoga unaweza kutumika kutengeneza mikate, chai, supu na dawa na kwenye vitu mbalimbali.
“Mfano Iringa wanalima uyoga na kuna uyoga ambao ni wa asili unapatika kwa msimu watu wanaukausha kwa namna ambayo ni ya asili na kuutumia wakati wote.
Alisema kuwa “kwa namna ya utafiti ambao tunafanya chuoni hapa uyoga huo utaboreshwa zaidi ili uweze kutumika na kupatikana mwaka mzima, uyoga utaandaliwa kwa namna ya kisasa ili utumike kwa namna mbalimbali kwenye vyakula na viungo mbalimbali”alisema
Alisema kuwa maonyesho hao yataleta tija kwa wakulima kwa sababu kupitia maonyesho hayo watajitangaza na kupata soko na elimu kwa wazalishaji wa uyoga ili wapate uelewa katika kulima kwa tija na masoko.
“Watapata mafunzo namna bora ya kulima uyoga kuuhifadhi, na matumizi mbalimbali kama chakula lakini pia watapata elimu ya masoko na kukutana na watafiti mbalimbali”
MWISHO.

