MWENGE WA UHURU WATAKA MRADI WA FORLAND KUSAIDIA ELIMU YA NISHATI SAFI MAKETE
Mwenge wa uhuru Mwaka 2026 umewataka wananchi wilayani Makete mkoani Njombe kuendeleza utamaduni wao wa kupanda miti na kuhifadhi mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kutumia nishati Safi.
Akiwa Iwawa wilayani Makete Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Mwaka huu Ndugu Wazo Mwang'onda wakati akikagua Banda la mradi wa uendelezaji Misitu chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland na Tanzania Forland amesema Kwa kuhifadhi mazingira kutawasaidia kupata hewa nzuri na nishati Safi ya kupikia.
Wakazi wa Makete akiwemo Samwel Mhema wanakiri kunufaika na elimu inayotolewa na mradi wa Forland ambao wanasema sasa watakwenda kuboresha Misitu Yao kwa kupanda mbegu za Kisasa ambazo zitawasaidia kujipatia kipato kwa muda mfupi.
Freeman Masawe Toka chuo Cha Misitu Tanzania na Careen Rita mtaalamu wa Misitu na viwanda vya Misitu Toka mradi wa Forland ambao wanasema kupitia mwenge wa uhuru wanatoa elimu ya uhifadhi mazingira na Misitu ili wakulima waweze kuzalisha kwa tija.




