Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MASHABIKI ARSENAL DODOMA WAFANYA SHEREH

MASHABIKI ARSENAL DODOMA WAFANYA SHEREH

 


Na Matukio Daima,Dodoma

Furahia na shamrashamra zimetawala jijini Dodoma baada ya mashabiki wa Arsenal kuungana kusherehekea ubingwa wa Ligi Kuu England walioupata msimu wa 2025/2026.

Mashabiki hao wameonekana wakifurahia mafanikio hayo kwa kula,kunywa na kucheza nyimbo mbalimbali kuisapoti timu yao huku wakisema ushindi huo ni wa kihistoria baada ya miaka mingi kupita bila kutwaa taji hilo.

Akizungumza katika mkusanyiko huo, Jerome Francis ambaye ni Mwenyekiti wa Mashabiki wa Arsenal Dodoma, amesema ushindi huo umeleta matumaini mapya kwa mashabiki wote wa klabu hiyo.

Mashabiki wengine akiwemo Peter Iman na Careen Winston wameeleza kuwa wamekuwa na subira kwa muda mrefu wakiamini siku moja timu yao ingerudi kileleni na kweli baada ya miaka 22 Hali hiyo imekuwa.

Wadau wengine wa soka waliokuwepo katika hafla hiyo pia wametoa maoni yao tofauti .



Shabiki wa Chelsea, Anselem Tairo, amesema Arsenal wameonyesha kiwango bora msimu huu na kustahili kuwa mabingwa ingawa hawana budi kulinda nafasi hiyo.


Kwa upande wake, Chomoka Chomoka amesema mashabiki wa Arsenal wanaamini huu ni mwanzo wa enzi mpya ya mafanikio ndani ya klabu hiyo.


Mwisho


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3