Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
FISTULA INATIBIKA? DAKTARI BINGWA AELEZA SABABU, DALILI NA TIBA”

FISTULA INATIBIKA? DAKTARI BINGWA AELEZA SABABU, DALILI NA TIBA”

 


Na Samwel Mpogole - Mbeya.

Katika kuadhimisha Siku ya Fistula Duniani, Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake Kutoka hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya Antidius Imanza ameitaka jamii  kuondoa unyanyapaa kwa wanawake wanaokumbwa na changamoto hiyo.

Akizungumza katika mahojiano maalum na matukio daima, daktari huyo amesema fistula husababishwa Sababu kuu zinazochangia tatizo hili ni pamoja na Uchungu wa muda mrefu, Kujifungua bila usaidizi wa kitaalamu. Mimba katika umri mdogo mbapo viungo vya uzazi na nyonga havijakomaa vizuri na Kuharibika kwa tishu wakati wa upasuaji wa uzazi au magonjwa mengine ya nyonga

Aidha, ameeleza kuwa ugonjwa huo unatibika iwapo mgonjwa atawahi hospitali na kupata matibabu kutoka kwa wataalamu, huku akisisitiza umuhimu wa jamii kuwapa faraja na msaada waathirika badala ya kuwanyanyapaa.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi waliozungumza na matukio daima wamesema elimu kuhusu fistula bado inahitajika zaidi katika jamii kwani wanawake wengi huishi kwa usiri kutokana na kuogopa kuchekwa au kutengwa.

Wananchi hao wameitaka serikali pamoja na wadau wa afya kuendelea kutoa elimu ya afya ya uzazi kuanzia ngazi ya familia hadi jamii, huku wakisisitiza umuhimu wa wajawazito kuhudhuria kliniki mapema ili kuepuka madhara yanayoweza kusababisha fistula.

Fistula ya uzazi ni tundu lisilo la kawaida linalojitokeza kati ya uke na kibofu cha mkojo au njia ya haja kubwa. Husababishwa na kuchelewa kupata huduma wakati wa kujifungua, ambapo shinikizo la muda mrefu la kichwa cha mtoto hukata usambazaji wa damu kwenye tishu za uzazi na kusababisha tundu hilo.

Maadhimisho ya siku hiyo yameelezwa kuwa ni sehemu muhimu ya kuikumbusha jamii kulinda afya ya mama na kuhakikisha wanawake wanaopata fistula wanapata matibabu na matumaini ya maisha bora.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3