UJUZI NI MALI, MTAJI VIJANA JITOKEZENI KURASIMISHA UJUZI WENU
Apr 22, 2026
Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda, amesisitiza kuwa ujuzi ni mali, mtaji na nguvu ya taifa, akiwataka vijana kujitokeza kwa wingi ili kutambuliwa na kurasimishwa ujuzi wao kwa lengo la kuongeza fursa za ajira ndani na nje ya nchi.
Akizungumza jijini Dodoma wakati wa uzinduzi rasmi wa Programu ya Mama Samia ya Utambuzi na Urasimishaji Ujuzi, Prof. Mkenda amesema kuwa serikali inatambua umuhimu wa ujuzi kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

“Kumpa kijana cheti cha ufundi stadi siyo kumpa karatasi tu, bali ni kumpa hadhi, sauti na nafasi ya kushindana kikamilifu katika soko la ajira ndani na nje ya nchi, " AmesemaProf. Mkenda
Ameongeza kuwa utekelezaji wa programu hiyo umezingatia urahisi wa upatikanaji wa huduma, ambapo mafundi na vijana wenye ujuzi hawatalazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma, bali watawasilisha maombi yao kupitia halmashauri au vyuo vya karibu vya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Aidha, amesisitiza kuwa mchakato mzima wa utambuzi na urasimishaji ujuzi umefadhiliwa kikamilifu na serikali, hivyo hakuna fundi atakayelazimika kulipia gharama yoyote.
Katika hatua nyingine, ameeleza kuwa si kila mwenye ujuzi atapewa cheti moja kwa moja, bali atafanyiwa tathmini kulingana na vigezo vilivyowekwa na VETA, na wale watakaobainika kuwa na mapungufu watapatiwa mafunzo ya ziada ili kufikia viwango vinavyotakiwa kabla ya kupewa vyeti vinavyotambulika rasmi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Anthony Kasore, amesema kuwa lengo la programu hiyo ni kuwafikia wananchi 80,000 ifikapo mwaka 2027.
“Kwa mwaka huu pekee, serikali imelenga kuwafikia wananchi 30,000, ambapo tayari fedha zimetolewa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi 14,400 bila malipo, " Amesema mkurugenzi Kasore
Aidha, amesema kuwa takriban shilingi milioni 600 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya programu hiyo, na kwamba baada ya kukamilika kwa awamu hiyo, jitihada zitaendelea ili kuwafikia wananchi waliobaki na kufikia lengo lililowekwa.
Programu hiyo inatarajiwa kuongeza ajira na fursa mbalimbali kwa wananchi baada ya kupata vyeti vinavyotambulika rasmi.

.jpg)