TEF WALAANI UVAMIZI OFISI ZA GAZETI LA PAMBAZUKO
Apr 11, 2026
Na Matukio Daima, Dar es salaam
Jukwaa la wahariri Tanzania TEF wamelaani tukio la kuvamiwa kwa ofisi za gazeti la Pambazuko na watu wasiojulikana ambao wameondoka na baadhi ya vifaa na nyaraka muhimu ikiwemo kompyuta.
Tamko hilo la maandishi limetolewa na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile kwa vyombo vya habari ambaye ametaka uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo kufanyika ili watuhumiwa wachukuliwe hatua Kali za kisheria.

