RPC NJOMBE:TUMEJIPANGA VIZURI SHEREHE ZA MEI MOSI
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limesema mkoa huo si wakufanya majaribio ya wizi wala vurugu kwani limejipanga vyema kuelekea sherehe za wafanyakazi duniani Mei mosi zinazotarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Njombe.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amesema kuelekea sherehe hizo jeshi hilo limeimarisha ulinzi na kuendelea na doria kila pahala hivyo yeyote atakayejaribu kujiingiza kwenye vitendo viovu atashughulikiwa.
Akiwa mkoani Dodoma mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amemhakikishia waziri mkuu kuwa maandalizi yanakwenda vizuri na hakuna kitakachoharibika katika sherehe hizo.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara mkoani Njombe wamesema wamejipanga vyema kuwapokea na kuwahudumia wageni wote walioanza kuingia mkoani Njombe kwa utangulizi wa michezo.
Shere za mei mosi kitaifa zinatarajiwa kufanyika mkoani Njombe ambazo huhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukusanya ugeni mkubwa.

