RAIS TRUMP AOKOLEWA MILIO YA RIASASI YASIKIKA NJE YA UKUMBI WA HOTEL
Taharuki imetanda jijini Washington baada ya milio ya risasi kusikika usiku wa leo wakati wa dhia ya kila mwaka ya waandishi wa habari wanaoripoti Ikulu ya Marekani (White House Correspondents' Dinner).
Rais Donald Trump aliondolewa jukwaani kwa haraka na kikosi cha usalama, huku yeye pamoja na mawaziri wake wote wakiripotiwa kuwa salama.
Mwandishi wa habari wa CNN, Wolf Blitzer, aliyekuwa nje ya ukumbi wa mikutano katika hoteli ya Washington Hilton, ameeleza kuwa alimwona mshambuliaji huyo akifyatua risasi hatua chache kutoka alipokuwa.
Blitzer alikuwa miongoni mwa makumi ya wageni waliojikita chini kujificha huku maofisa wa usalama wakivamia eneo hilo.
Rais Donald Trump ameeleza kuwa mshukiwa mmoja aliyekuwa na "silaha kadhaa" alijaribu kupita kwa nguvu katika eneo la ukaguzi wa usalama kabla ya milio ya risasi kusikika.
Rais alikatisha hotuba yake na kukimbizwa nje ya ukumbi na maofisa wa usalama kwa ajili ya usalama wake.
Mshukiwa wa tukio hilo tayari anashikiliwa na polisi. Mwanasheria wa Marekani katika Jimbo la Columbia, Jeanine Pirro, amesema mshukiwa huyo atakabiliwa na mashtaka ya kutumia silaha ya moto kufanya uhalifu na kumshambulia ofisa wa serikali kwa silaha hatari.
Maofisa wa usalama wamemtambua mshukiwa kuwa ni mwanamume mwenye umri wa miaka 31, mkazi wa jimbo la California.



