Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MWENEZI KAGERA ASISITIZA WANACHI KUDUMISHA AMANI

MWENEZI KAGERA ASISITIZA WANACHI KUDUMISHA AMANI

 


Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera 

Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera 

Katibu wa siasa uenezi na mafunzo wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Kagera,  Hamim Mahmoud amesisitiza wananchi wa mkoa wa Kagera kudumisha Amani na utulivu katika maeneo yao ili kuruhusu shughuli za maendeleo kufanyika.

Akizungumza wakati wa bonanza la mchezo wa miguu lililofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Kashai manispaa ya Bukoba lililoandaliwa na umoja wa vijana wa  chama cha mapinduzi UVCCM kata ya Kashai,  Hamim ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kuwa bila Amani hata shughuli za michezo haziwezi kufanyika.

"nisistize Amani na utulivu nchini bila Amani hata shughuli za michezo hatuwez kuzifanya watu wote atuwezi kukusanyika bila Amani kuwepo hili ni suala muhimu tudumishe amani"


Aidha katika bonanza hilo mwenezi ameahidi seti mbili za jezi kwa timu ya kata  Kashai na pia amesisitiza kuendelezwa kwa vipaji vya vijana wa kata ya Kashai ili kukuza michezo na kutengeneza ajira kwa vijana kupitia mchezo wa mpira wa miguu.

"nimeulizia bei ya jezi wameniambia ni kama shilingi laki mbili niahidi mwezi wa sita nitaleta seti mbili za jezi kwa timu ya Kashai lakini limezungumzwa suala la kuinua vipaji vya vijana kupitia mabonanza haya na ligi hizi kunaibuliwa vipaji vingi kama akina Kibu Denis ametoke kwenye ligi ya jimbo cup hapa kwa sasa yupo huko uarabuni anapata pesa"


Katika hatua nyingine kiongozi huyo wa CCM Kagera ameitaka Halmashauri ya manispaa ya Bukoba kuboresha uwanjwa wa shule ya msingi Kashai maji yasituame kwenye uwanja na hivyo kuruhusu shughuli za michezo kufanyika katika uwanja huo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa UVCCM kata Kashai Abdulrazack Mohamed ameomba kuwasaidia vijana wenye vipaji hasa vya mpira wa miguu waweze kupata timu za kuchezea kama Kagera Sugar na hivyo kupata ajira na kuinuka kiuchimi.

"mheshimiwa mgeni rasmi niombe kuwasaidia vijana wenye vipaji katika kata yetu ya Kashai waweze kuendelezwa na kupata timu za kuchezea"



Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3