MAGONJWA YA MGONGO NA UBONGO YAONEKANA KUWA NI CHANZO CHA VIFO KWA WATU.
Apr 22, 2026
Na,Jusline Marco;Arusha
Takribani vifo 56000 hutokea Kila mwaka kutokana na magonjwa yasiyo ya kuambukizila ikiwemo magonjwa ya mgongo, uti wa mgongo, mishipa ya fahamu, ubongo na kichwa ambayo ndiyo miongoni mwa sababu kuu za vifo.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani Dkt. Vaneshwar Ashok ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kambi ya matibabu ya kibingwa kwa magonjwa ya moyo,ubongo na mgongo itakayofanyika April 28 hadi tarehe Moshi mwezi Mei mwaka huu jijini Arusha chini ya madaktati kutoka matekani na Tanzania.
Dkt. Ashok amesema magonjwa hayo mara nyingi watu huwa nayo bila kuonyesha dalili zozote huku akieleza kuwa idadi kubwa ya wahpnjwa bado awajagindulika ambapo amesema kuwa kati ya asilimia 25 mpaka 40 ya watu wazima nchini wanashinikizo la damu huku wengi wao wakiwa bado hawajagundulika.
Aidha amesema magonjwa hayo kama shinikizo la damu lisipogundulika mapema linaweza kusababisha madhara makubwa kama kiharusi, shambulio la moyo , moyo kushindwa kufanya kazi , figo kuharibika na hata kusababisha kifo cha hafla.
Ameongeza kuwa nchini Tanzania lipo ongezeko kubwa la magonjwa ya mgongo ambapo watu wengi huishi na maumivu ya mgongo na shingo kwa muda mrefu kutokana na hali ambayo inaweza kusababisha maumivu na hupunguza uwezo wa kufanya kazi na shughuli za Kila siku.
Amebainisha kuwa utambuzi wa mapema husaidia kuzuia madhara makubwa, kupunguza ulemavu na kuboresha ubora na hali ya maisha ambapo ametoa wito kwa wakazi wa Kanda ya Kaskazini na Tanzania kwa ujumla kutumia fursa ya uwepo wa kambi hiyo kujitokeza kupima afya zao.
Awali Meneja Miradi kutoka Tanlink Medical Tourism Agency, Baraka Fales amesema kuwa Taasisi hiyo ya kitanzania, inajihusisha katika kusimamia na kuratibu matibabu ya binadamu ndani na nje ya nchi, imekuwa kusaidia wagonjwa kupata madaktati husika na kwa wakati ambapo katika kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanlink imekuja na wazo la kuratibu na kusimamia kambi za matibabu na madaktati bingwa kutoa matibabu nchini.
Amesema Tanlink kwa kushirikiana na Hospitali ya The Aha Khan Tanzania imewaandalia wananchi wa Mkoa wa Arusha kambi ya matibabu bayo itahusisha watu wote wenye changamoto za magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo moyo na presha, pamoja na wale wasiokuwa na changamoto ambao wanatamani kufanya vipimo ili kujua afya yao ya mwili.

