Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MADIWANI BUKOBA WALIA NA UBOVU WA BARABARA

MADIWANI BUKOBA WALIA NA UBOVU WA BARABARA

 

Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera

Madiwani wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wameutaka Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kuzifanyia ukarabati barabara za mitaa katika maeneo yao, wakisisitiza kuwa hatua hiyo itarahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa, hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi.

Hayo wameyabainisha katika kikao cha baraza la madiwani ambapo Diwani wa Kata ya Bilele Tawfiq Sharifu ametaka kuzibwa kwa mashimo katika barabara zilizopo katika kati ya mji wa Bukoba ambazo hazileti taswira nzuri ya mji huo.

“mheshimiwa mstahiki meya kikao cha maendeleo ya kata tunaomba kuzibwa kwa mashimo katika barabara ya Kawawa na barabara ya Arusha kwakweli mashimo ya barabara hizo yanatia kichefu chefu na hayaleti taswira nzuri ya m ji wetu”

Kwa upande wake diwani wa kata ya Kibeta Anastella Alphonce ameeleza kuwa kila mara wamekuwa wakibainisha barabara mbovu katika maeneo yao lakini hazifanyiwi ukarabati hali inayopelekea ugumu kwa wananchi katika ufanyaji wa shughuli za kuwaingizia kipato.


“ninawaomba TARURA watusaidia hasa wananchi wa Busisi na Bugezi hali ya barabara ni mbaya wananchi wanashindwa kutoka kutokana na ubovu wa barabara tunaomba mtufanyie ukarabati kwa haraka”

Kwa upande wake meneja wa TARURA manispaa ya Bukoba Mhandisi Emmanuel Yohana amesema kuwa barabara nyingi ambazo zimeanishwa katika baraza hilo tiyari zimetengewa bajeti ya matengenezo katika mwaka wa fedha 2026/2027.

“mheshimiwa mstahiki Meya ni kweli kutokana na mvua hizi zinazoendelea kunyesha barabara nyingi zimeharibika lakini niwakumbushe madiwani barabara hizi katika mwaka wa fedha 2026/27 zimetengewa bajeti na zitatekelezwa kwahiyo niwahakikishie madiwani barabara zitatengenezwa.

Akizungumza katika baraza hilo mkuu wa wilaya ya Bukoba amewataka madiwani kusimamia shughuli za maendeleo zinazotekelezwa katika maeneo yao ili kuleta matokeo chanya yaliyokusudiwa na serikali ya kuwahudumia wananchi.

“msimamizi mkubwa wa miradi yote ni mkurugenzi wa manispaa hii, kwahiyo kama mradi unaotelekelezwa katika kata hizi ipo chini yake mnatakiwa kuisimamia ili malengo ya serikali yafikiwe”

Jumla ya shilingi bilioni 2.8 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara katika manispaa ya Bukoba kwa mwaka wa fedha 2026/2027 hali inayotarajia kuwaondolea adha ya usafiri wananchi kwa kiasi kikubwa.

MWISHO.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3