Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
LUSEKELWA, TUSHEREHEKEA PASAKA KWA NJIA INAYOTUKUZA MUNGU.

LUSEKELWA, TUSHEREHEKEA PASAKA KWA NJIA INAYOTUKUZA MUNGU.

 


NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA MWANZA.

MWANZA, Askofu Mkuu wa makanisa ya C.E.C Tanzania, Charles Sekelwa, amewataka waumini wa dini ya Kikristo nchini kusherehekea Pasaka kwa njia inayomtukuza Mungu kwa kufanya matendo ya huruma kwa watu wengine na sio kusherehekea kwa mitindo ya dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprilini 2, 2026 ofisini kwake Jijini Mwanza, Askofu Sekelwa alisema kuwa Pasaka ni kipindi cha ukombozi kwa waumini, ambapo wanakumbuka mateso, kifo, na ufufuo wa Yesu Kristo. 

Kwa mujibu wa Askofu Sekelwa, ameeleza kuwa matendo mema yanayoonyeshwa wakati wa Kwarezima, kama vile kusaidia wahitaji, kutubu, na kujinyima, hayapaswi kumalizika baada ya Pasaka hivyo kila muumini anapaswa kuendelea kuyaenzi na kuyaishi mambo hayo kwa watu wote hata baada ya pasaka.

"Pasaka ni wakati wa kutafakari na kumshukuru Mungu kwa upendo mkubwa alioonyesha kwa kumtuma mwanae Yesu Kristo kuja kufa kwa ajili ya dhambi zetu, hivyo tunaposherehekea Pasaka, tunapaswa kutafakari kwa undani kuhusu dhabihu ya Yesu, na jinsi tunavyoweza kuishi maisha yanayomtukuza Mungu," alisema Askofu Sekelwa.

Aidha amesisitiza kuwa Matendo mema yanapaswa kuendelea baada ya Pasaka na hivyo wakristo hawapaswi kuyaacha matendo mema katika kipindi cha Kwarezima pekee, hivyo wanapaswa kuwa ni maisha yao kila siku, kwani kufanya matendo mema ni njia bora ya kumuenzi Yesu.

Kwa upande mwingine, Askofu Sekelwa amewakumbusha waumini kuwa sherehe za Pasaka hazipaswi kuchanganyikana na matendo yasiyofaa kama vile ulevi, uzinzi, na mayendo mengine maovu yanayomchukiza Mungu.

 "Pasaka ni wakati wa kutafuta mabadiliko ya kiroho na siyo wakati wa kusherehekea kwa mtindo wa dunia. Tunaposherehekea Pasaka, tunapaswa kuwa na nia ya kweli ya kumtukuza Mungu na kumuenzi Yesu kwa matendo mema," alisema.

Askofu Sekelwa aliendelea kusema kwamba Pasaka inatoa nafasi kwa Wakristo kujiweka huru kutoka kwa dhambi na kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3