Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
CCM YASHAURI MAMBO SITA KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA

CCM YASHAURI MAMBO SITA KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA

 


Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media, Dodoma 

KUFUATIA bei ya mafuta kupanda Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeishauri Serikali mambo sita ikiwemo kuanzishwa kwa mfuko maalumu wa kudhibiti bei za mafuta ili kupunguza athari za mabadiliko ya ghafla ya bei katika soko la dunia. 


Ushauri huo umetolewa leo April 7,2026 na Katibu wa Itikadi, Uenzi na Mafunzo, Kenani Kihongosi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto ya kupanda kwa bei ya mafuta nchini.


Kihongosi  alisema kuwa CCM inashauri kuanzishwa kwa mfuko maalumu wa kudhibiti bei za mafuta ili kupunguza athari za mabadiliko ya ghafla ya bei katika soko la dunia. 


Pia,inashaudi  umuhimu wa kuwa na akiba ya kimkakati ya mafuta ili kuhakikisha upatikanaji wake unaendelea kuwa wa uhakika wakati wote.


Vilevile,Kihongosi ameitaka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kusimamia kikamilifu sekta ya mafuta ili kuzuia uchepushaji na kuhakikisha mafuta yanapatikana kwa uwazi na ufanisi.


Pia, amehimiza uwekezaji zaidi katika miundombinu ya kuhifadhi mafuta na kuongeza vituo vya mafuta kwa kushirikiana na sekta binafsi.


“Kuhusu sera za nishati, serikali inapaswa kuangalia uwezekano wa kutoa ruzuku kwenye mafuta pamoja na kuhimiza matumizi ya nishati mbadala, hususan gesi asilia, ili kupunguza utegemezi wa mafuta ya nje,” amesema Kihongosi.


Vilevile, amesisitiza umuhimu wa kuanzishwa kwa mfuko wa kuendeleza utafutaji na uchimbaji wa mafuta nchini ili kuhakikisha taifa linakuwa na uhakika wa nishati kwa muda mrefu.


Kihongosi pia amewataka Watanzania kutambua kuwa kupanda kwa bei ya mafuta ni hali ya dunia nzima na si suala la kisiasa, huku akisisitiza kuwa pamoja na wito wa kupunguza baadhi ya tozo, ushuru ni muhimu katika kugharamia maendeleo ya nchi.


Mwisho

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3