BODABODA WAPANDISHA NAULI BUKOBA
Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera
Kufutia ongezeko la bei ya mafuta ya petroli na dizeli nchini bei za usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda mjini Bukoba zimepanda kwa zaidi ya asilimia mia moja kutoka sehemu moja hadi nyingine hali inayoleta adha kwa wananchi.
Wakizungumza na Matukio Daima Media wananchi hao akiwemo Ashura Jumapili wameeleza kuwa kwa sasa wanapata wakati mgumu kusafiri kutoka eneo moja hadi nyingine kutokana na kupanda kwa nauli na kuwalazimu wengine kutembea kwa miguu kutokana na ugumu wa maisha.
“nauli zimepanda kwa asilimia mia moja sehemu ambayo ulikuwa unaendea kwa shilingi elfu moja kwa sasa ni shilingi elfu mbili mpaka shilingi elfu nne kwahiyo kila bodaboda ana nauli yake kwa sasa na inatumiza sisi wananchi”
Aidha Ashura ameiomba serikali idhibiti upandaji holela wa nauli kwani inawaumiza wananchi wa kipato cha chini na pia ameiomba serikali kuona namna ya kushusha gharama za mafuta ili kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi kutokana na kupanda kwa bidhaa nyingi ikiwemo za vyakula.
“ukiangalia nauli za mabasi ya kwenda mikoani hazijapanda kwanini hawa bodaboda wapandishe nauli serikali ione namna ya kudhibiti kupanda holela kwa nauli iwawekee bei maalumu kwasababu vituo vyao vinajulikana”
Kwa uapande wake mwendesha pikipiki (bodaboda) Ibaada Amada amesema kuwa sababu ya wao kupandisha nauli ni kutokana na kuapanda kwa bei ya mafuta ndio maana na wao wameamua kupandisha nauli ili na wao wapate faida.
“sehemu tuliyokuwa tunaendea kwa shilingi elfu moja kwa sasa tumepandisha kidogo mpaka elfu moja na mia tano mpaka elfu mbili ni kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta na sisi hatuna jinsi japo wateja wengine wanakataa kupanda pikipiki wanatembea kwa miguu”
Naye dereva wa tax ya kukodishwa Renatus Kateme amesema kuwa kwa sasa wanapata ugumu wa biashara ya usafirishaji wa abiria kutokana na baadhi ya wananchi kukataa bei mpya wanazoambiwa na hivyo kukosa abiria.
“kupanda kwa bei ya mafuta umetuathiri sisi madereava tax, sehemu tulipokuwa tunaendelea kwa shilingi elfu Hamsini kwa sasa ni elfu themanini ila akija abiria ukamwambia anakataa unaona mpaka sasa hatuna abiria toka asubuhi”
Itakumbukwa April mosi mwaka huu mamlaka ya uthibiti wa nishati na maji EWURA ilitangaza ukomo wa bei mpya za mafuta zikiwa na ongezeko la zaidi ya shilingi elfu moja kwa lita ambapo kwa mji wa Bukoba mafuta ya petroli ni shilingi elfu nne na sabini huku Diseli ikiwa ni shilingi elfu nne na hamsin na sita.
