BUKOBA YAFANYA VIZURI KATIKA KURIPOTI NA UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI SHULENI
Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera
Mkuu wa wilaya ya Bukoba Mkaoani Kagera Erasto Sima amesmea kuwa hali ya uandikishaji na kuripoti kwa wanafunzi wa darasa la kwanza,awali na sekondari ni nzuri katika wilaya hiyo kutokana na ijtihada za wazazi na viongozi wa serikali ngazi za chini.
Akitoa takwimu za zoezi la kuripoti na uandikishwaji wa wanafunzi kwa shule za sekondari na shule ya msingi lililokamilika March 31 mwaka huu, Sima ameeleza kuwa kwa shule za sekondari hali ya kuripoti kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa halimashauri ya wialaya ya Bukoba ambayo ina shule 38 ni asilimia 99 huku darasa la kwanza aliojiandikisha ni sawa na asilimia 133 na darasa la awali waliojiandikisha nis awa na asilimia 124 ya maoteo ya uandikishaji.
“jana tarehe 31 mwezi wa 3 tumekamilisha takwimu za uandikishaji na kuripoti kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kama maelekezo tuliyopewa, katika halmashauri ya Bukoba tunazo shule za sekondari 38, wanafunzi walioripoti kidato cha kwanza ni asilimia 99 kulingana na maoteo ya kuripoti kwa wananfunzi hao katika shhule mbalimbali”
Aidha mkuu huyo wa wilaya ameeleza kuwa kwa manispaa ya Bukoba yenye shule za sekondari 20 hali ya kuripoti kwa wanafunzi ni sawa na asilimia 100, huku kwa madarasa ya awali walioandikishwa ni sawa na asilimia 73.3 na darasa la kwanza waliondikishwa ni sawa na asilimia 98 ya maoteo yote.
“katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba tunazo shule za sekondari 20 katika shule hizo za sekondari wanafunzi waliokwisha ripoti ni sawa na asilimia 100 maana wote walitakiwa kuripoti wamelipoti na tayari wameishaanza masomo na kwa madarasa ya awali uandikishwaji ni sawa na asilimia 73.3 na hii inatokana na manispaa ya Bukoba kuwa vituo vingi vya kulea watoto”
Hata hivyo kiongozi huyo wa wilaya amewapongeza wazazi na watendaji wa serikali katika ngazi ya Kata, vijiji na mitaa katika kuhakikisha wanafunzi wanajiandikisha na kuripoti katika shule za walizopangiwa huku akieleza kuwa wataendelea kuwafuatilia wanafunzi ambao bado hawajaripoti shule kuhakikisha wanaripoti shule.
Itakumbukwa kuwa muhula mpya wa masomo wa mwaka 2026 ulifunguliwa Januari 13, 2026.




