BAJETI YA WIZARA YA MADINI 2026/2027 YALENGA KUIMARISHA MAPATO NA USIMAMIZI WA RASILIMALI
Apr 27, 2026
Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma
WIZARA ya Madini imewasilisha ombi bungeni la kuidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 174.98 kwa ajili ya mwaka wa fedha 2026/2027, fedha zitakazotumika kutekeleza majukumu mbalimbali ya sekta hiyo.
Akiwasilisha makadirio hayo Aprili 27, 2026, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, alieleza kuwa sehemu ya fedha hizo, takribani shilingi bilioni 71.51 sawa na asilimia 40.87, imepangwa kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Kwa upande mwingine, kiasi cha shilingi bilioni 103.47, sawa na asilimia 59.13 ya bajeti yote, kimetengwa kwa matumizi ya kawaida ya wizara pamoja na taasisi zilizo chini yake. Ndani ya fungu hilo, shilingi bilioni 27.36 zitatumika kulipa mishahara ya watumishi, huku shilingi bilioni 76.11 zikigharamia shughuli nyingine za kiutendaji.
Waziri Mavunde alisisitiza kuwa utekelezaji wa bajeti hiyo utachangia kuimarika kwa ukusanyaji wa mapato ya serikali, yakilenga kufikia shilingi trilioni 1.4, sambamba na kuboresha usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za madini nchini.
Mwisho
