AJALI YA BASI NA GARI DOGO YAUA
Apr 26, 2026
Watu watatu wanahofiwa kufariki dunia katika ajali iliyohusisha magari mawili yenye namba za usajili KDV151G aina ya SCANIA Bus (TAHMED) na DFPA 2191 TOYOTA LAND CRUISER baada kukogana uso kwa uso usiku wa leo majira ya saa sita usiku (00:00) katika Eneo la Same Mjini barabara kuu ya Tanga/Moshi.
Chanzo cha ajali inadaiwa ni uzembe wa dereva wa gari aina ya TOYOTA LAND CRUISER iliyokuwa inatokea uelekeo wa Moshi kuhama upande wake wa kushoto na kwenda upande wa kulia wa barabara bila tahadhari kisha kugongana na Bus kampuni ya TAHMED iliyokuwa inatokea Dar es Salaam kwenda Namanga.
Watu watatu wanaohofiwa kupoteza maisha waliokuwa kwenye TOYOTA LAND CRUISER, majeruhi wawili ambapo mmoja alikuwa kwenye gari LAND CRUISER na mwingine kwenye Bus na wote wamekimbizwa katika Hospital ya Wilaya Same kwa ajili ya matibabu.
