Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WIVU WA MAPENZI NA ULEVI CHANZO CHA MAUAJI KAGERA

WIVU WA MAPENZI NA ULEVI CHANZO CHA MAUAJI KAGERA

 


Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kagera Blasius Chatanda amesema kuwa mkoa huo bado una kiwango cha juu cha mauaji kwa miaka ya hivi karibuni huku chanzo kikubwa cha matukio hayo ikiwa ni wivu wa mapenzi, ulevi uliopitiliza na migogoro ya Aridhi.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda Chatanda amesema kuwa kwa mwaka 2025 matukio ya mauaji yaliyoripotiwa yalikuwa 134 yakilinganishwa na matukio 182 mwaka 2024 ambapo ni kwa kiwango cha juu ukilinganisha na mikoa mingine.

"kwa mwaka 2025 kulikuwa na matukio ya mauaji 134, unaweza kuona kuna upungufu wa matukio 48 na hizo ni jitihada ambazo tumefanya katika kuthibiti matukio ya mauaji na kazi kubwa hasa tulioifanya ni kuongeza upelelezi wa matukio hayo"

Aidha katika hatua nyingine kamanda huyo ameeleza kuwa kwa mwaka 2025 kulikuwa na matukio 290 ya ubakaji na matukio 17 katika mkoa wa Kagera ikiwa ni pungufu ya matukio 9 ukilinganisha na matukio 26 kwa mwaka 2024.

"katika mkoa wetu pia bado kuna matukio ya ubakaji hasa kwa watoto wadogo ambapo kwa mwaka 2024 kulikuwa na matukio ya kubaka 325 na mwaka 2025 kulikuwa na matukio 290 lakini pia kwa mwaka 2025 kumeripotiwa matukio 16 ya ulawiti"

Akitaja hatua zilizochukuliwa kwa watu waliohusika na matukio ya mauaji kwa mkoa wa Kagera kamanda huyo ameeleza kuwa watuhimiwa 4 kati ya watano wamehikumiwa kunyongwa hadi kufa na watuhimiwa sita wamehikumiwa kifungo cha miaka thelathini jela.

Hata hivyo kwa upande wa watuhimiwa wa kubaka watu 24 wamehikumiwa kifungo cha maisha jela na watu 62 wamehikumiwa kifungo cha miaka thelathini jela na watu wawili waliohusika na matukio ya kulawiti wamehikumiwa kifungo cha maisha jela.

"watu 24 wamehikumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka  na watu 62 wamehikumiwa kifungo cha miaka thelathini jela na watu wawili waliohusika na matukio ya kulawiti wamehikumiwa kifungo cha maisha jela huku watu 4 wa kesi za kulawiti wamehikumiwa kifungo cha miaka thelathini jela"

Kadhalika kamanda huyo wa jeshi la polisi mkoa wa Kagera amewataka wazazi na walezi mkoani humo kuwa makini na watoto wao na kuacha kuwaamini watu kupitiliza na kuwaachia watoto hali inayopelekea baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema kufanya matendo ya ubakaji na ulawiti kwa watoto.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3