Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WANAHABARI MWANZA WAOMBWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA WADAU

WANAHABARI MWANZA WAOMBWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA WADAU

 

NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA MWANZA.


MWANZA, Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza wamehimizwa kuendelea kujenga na kudumisha ushirikiano na wadau mbalimbali ili kuchochea maendeleo ya sekta zao na jamii kwa ujumla.


Rai hiyo imetolewa Machi 19, 2026 jijini Mwanza na Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji wa Malori ya Masafa Marefu na Mabasi ya ndani na nje ya nchi(TLDTA), Hassan Dede, wakati wa hafla ya Iftar iliyoandaliwa kwa wanahabari wa mkoa huo.

Dede amesema ushirikiano kati ya wanahabari na wadau wa sekta ya usafirishaji una nafasi kubwa katika kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo na utoaji wa taarifa sahihi kwa umma.


Amesema waandishi wa habari wana mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yao hivyo ameona ni vyema kujumuika nao pamoja kama ishara ya umoja, mshikamano na upendo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma.


"tukio hili la Iftar limeandaliwa kama sehemu ya kuimarisha mahusiano na kuthamini mchango wa wanahabari katika kazi zao za kila siku" Alisema Dede.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Binagi Media, George Binagi, amesema ushirikiano uliopo umeendelea kuleta matokeo chanya na mafanikio katika mkoa huo.


Binagi amesisitiza umuhimu wa wanahabari kushiriki katika masuala yanayohusu jamii yao pamoja na kuendeleza mshikamano miongoni mwao.


“Ni muhimu pia kukumbushana wajibu wetu wa kijamii. Mara nyingi tumekuwa mstari wa mbele kuripoti matukio ya wengine, lakini tusisahau kushiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii yanayotuhusu sisi wenyewe,”amesema Binagi





Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3