BODABODA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Polisi Mkoa wa Kigoma inafanya uchunguzi wa kifo cha Joseph Gidion Filimon (30) dereva pikipiki na mkazi wa Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji aliyeuawa kwa kuchomwa na kisu eatu wasiojulikana.
Awali wananchi wanaoishi jirani na marehemu walimtuhumu mwanamke aliyekuwa akiishi na bodaboda huyo ambaye anaelezwa kumfikisha marehemu Hospitali y rufaa ya mkoa Kigoma Maweni na baadaye kutoweka huku akizima simu zake zote.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Filemon Makungu akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kugoma alisema kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo, huku akitoa wito kwa yeyote mwenye taarifa muhimu kujitokeza kusaidia uchunguzi huo.
Akizungumzia tulio hilo Baba mzazi wa marehemu, Gidion Philemon amesema familia imeachwa na maswali mengi, akieleza kuwa mwanamke aliyekuwa akiishi na mwanawe alimfikisha hospitalini kisha kutoweka kusikojulikana na hazipatikani hadi sasa na simu zake zimezimwa.
Mzee Philemoni alisema kuwa alipigiwa simu na mwanamke huyo akielezwa kuwa mwanawe alichomwa na kitu nyenye ncha kali kwenye Bega lake la kulia na watu wasiojulikana ambo linalozua utata zaidi kuhusu tukio hilo.

