UVIKO-19 TISHIO WANAFUNZI IRINGA WAPEWA ELIMU KUHUSU KUEPUKA UGONJWA HUU
Na Easter Kameta, UoI
Matukio Daima Media
Ugonjwa wa UVIKO-19, unaosababishwa na virusi vya SARS-CoV-2, unaendelea kuenea kwa kasi, hasa kupitia njia ya hewa. Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa wametolewa elimu kuhusu ugonjwa huu na njia za kuepuka maambukizi.
Katika hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya wanafunzi, Waziri Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa, Rashid Mdee, aliwaasa wanafunzi kuepuka mikusanyiko ili kujilinda dhidi ya ugonjwa huu, akieleza namna unavyoenezwa na kuonya kwamba hali inavyozidi kuwa mbaya, ndivyo maambukizi yanavyozidi kuongezeka.
“Ugonjwa huu unaenea kwa kasi, hasa kwa watu walio katika mikusanyiko Watu walio katika hali ya kukutana kwa karibu wana hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu, kwani kirusi kinaenea kupitia njia ya hewa. Kwa mfano, mtu anapokoa au kuharisha, virusi vinaweza kuenea hewani na kumfikia mtu mwingine, hivyo kuleta maambukizi,” alieleza Mdee.
Schola Mbisa, mtaalamu wa afya, alizungumzia dalili za ugonjwa huu, akisisitiza kuwa dalili za awali ni uchovu wa mara kwa mara na upungufu wa nguvu mwilini.
“Mtu aliyeathirika na UVIKO-19 anaweza kujikuta akichoka kila wakati, kuwa na homa kali, kukohoa mara kwa mara, kupoteza uwezo wa kunusa au ladha ya vitu, na kupumua kwa shida. Ugonjwa huu hushambulia sana mfumo wa upumuaji,” alisema Schola.
Christina Reubeni, mtaalamu mwingine wa afya, alitaja njia bora za kuepuka maambukizi ya UVIKO-19, akisisitiza umuhimu wa kuvaa barakoa, kunawa mikono mara kwa mara kwa maji safi na sabuni, pamoja na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.
“Ili kujikinga na maambukizi ya UVIKO-19, ni muhimu kuvaa barakoa kila wakati, kunawa mikono mara kwa mara, na kuepuka mikusanyiko na safari zisizo za lazima,” alisisitiza Reubeni.
Mtaalamu wa afya Anastazia Mwakasege pia alikumbusha wanafunzi kuwa na makini na dalili za ugonjwa huu na kumhimiza kila mmoja kuvua barakoa na kwenda hospitali mara moja wanapoona dalili za UVIKO-19.
“Wanafunzi, ni muhimu kuvaa barakoa muda wote mnapo kuwa madarasani. Ninyi ni mfano kwa jamii, na ni jukumu lenu kuhamasisha matumizi ya barakoa na kuhakikisha kuwa watu wanapojihisi kuwa na dalili za ugonjwa huu, wanakwenda hospitalini kwa uchunguzi na matibabu,” alisema Mwakasege.
Elimu hii imejikita katika kuwasaidia wanafunzi kuendelea kujilinda na kuepuka kuenea kwa ugonjwa wa UVIKO-19, ambao bado unahatarisha afya za watu wengi.

