Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
UMUHIMU WA WAUMINI KUFUNGA NA FAIDA ZAKE

UMUHIMU WA WAUMINI KUFUNGA NA FAIDA ZAKE

 


NA EASTER KAMETA (UoI)

MATUKUO DAIMA

 Waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu mkoani Iringa wahimiza juu ya suala kufunga hasa msimu huu wa kwaresma na ramadhani pia wataja baadhi ya faida atazo zipata mtu iwapo atafunga.

Akizungumza,na matukio daima Abuubakar Omarry ameeleza maana ya ramadhani ,huku akitaja baadhi ya baadhi ya matendo ambayo mtu hapaswi kuyanya mda wa funga kama vile kufanya matendo ya kiovu 


"Ramadhani hii nifunga ya kumkarbia mwenyezi mungu kwa njia ya kufunga pia msimu huu wa ramadhani muumini hipaswi kufanya matendo yasiyo faa wala yasiyo  mpendeza mwenyezi mungu matendo hayo kama ulevi ,wizi ,dhuruma ukifanya hivyo utakua umeenda kinyume na mwenyezi mungu pia umeharibu funga yako kama muhislam."

 Isaac Abasi ameeleza maana ya  kwaresma huku akitaja kuwa kupitia kwaresma watu wengi wanapata kumkaribia mungu pia ametaja kuwa kwaresma ni chachu ya watu kuwa na maadili mema.

"Msimuu huu wa kwaresma wakristo tunaufanya kama mwezi ambao unatukutanisha kati ya mwanadamu na Mungu pia kwaresma inawahimiza watu kufanya yaliyo mema kama vile kuhimiza watu  kumtumaini Mungu kuwa  na upendo na kudumisha amani na kudumisha maadili mema Pia kupiga vita mambo yanayo  kwenda kinyume na dini kama vile uasherati  ,ushirikina"

Mwanahamisi  Hamisi ameeleza baadhi ya faida ambazo mtu aliye funga atazipata  Huku akitaja kuwa faida hizi atazipata katika upande wa afya ya mwili na katika upande wa kiroho akitaja kuwa watu wataimarika  zaidi.

"Mtu aliye funga ataimarika kiroho pia nafsi yake itakuwa ikitaja hasa mambo yaliyo mema pia katika afya ya mtu aliye funga itakuwa salama kwasababu mmeng'enyo wa chakula utakaasa ,mwili kuwa mwepesi pia ataepuka baadhi ya  magonjwa  kama vile homa ya matumbo, unene kupitiliza ,presha  ,kisukari"

Rahma Hassan amewataka waumini wote wapate kufunga ili kuepuka baadhi ya mambo huku  akishauri jamii na watu wake kwa kuwaonyesha baadhi ya mambo ambayo wanapaswa kufanya msimuu huu wa hizi funga zote mbili.

"Jamani tufunge kuanzia matendo hadi roho na nafsi zetu kwani mtu ikiwa umefunga afu unasengenya hapohujafunga weendelea kula tu pia  mtu unapo funga hupaswi kufanya vitu ambavyo viko kinyume na maadili ya dini kama ulevi ambao hufanya mtu kufanya vitu vya kikatili, watu wanapaswa kuwa na lugha nzuri ya ukarimu na ushilikiano  upendo kwa watu wote na dini zote ubaguzi haufai"

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3