ADHARA YA VIJANA KUTUMIA POMBE WAKIWA NA UMRI MDGO
Na Catherin Kilwale (UoI)Matukio Daima Media.
Mganga Mkuu wa Zahanati ya Ngome Kata ya Kihesa Mkoani Iringa, John Mlunguza ameleza kuwa matumizi ya pombe kupita kiasi kwa baadhi ya vijana yamekuwa changamoto katika jamii,kwanii yanapelekea vijana wengi kuathirika kiafya.
Amesema kuwa vijana wengi wa kizazi hichi wanatumia pombe kali pasipo kujua zinaleta athari gani katika mwili,pia wengine husema kuwa zinapunguza mawazo kwani kwa uhalisia pombe haipunguzi mawazo.
"Vijana wanaotumia pombe wa kiwa na umri mdogo wanaweza kuathirika kiafya, kama vile kijana anaweza kupata ugonjwa wa Ini, kuathiri ubongo na kumbukumbu pia anaweza kupata vidonda vyatumbo na hata kupunguza kinga za mwili dhidi ya magonjwa, kutokana na matumizi ya vileo vikali.
Kwa upandewake Emmanuel Msigwa ambaye ni kijana wa Kata hiyo ,amesema kuwa kutokana na utandawazi wa sikuizi vijana wengi hushawishika kutumia pombe kali wakiwa na umri mdogo wakidhani kuwa nisalama kiafya.
"Baadhi ya vijana hutumia pombe pale wanapokuwa na msongo wa mawazo,wakiamini kuwa pombe ndio njia pekee ya kuondoa mawazo pia wengiwao hutumia pombe kwa kuiga makundi mabaya ya mtaani".
Huku Getruda Bulinje ambaye ni mkazi wa kata ya kihesa,amesema kuwa katika jamii yetu vijana wengi hutumia pombe wakiwa na umri mdgo kutokana na kukosa malezi bora kwa wazazi, kwani hupelekea vijana haokujiona wanacho kifanya nisahii.
"Kutokana na janga hili la vijana kutumia pombe husababisha athari kubwa katika jamii kana vile, vijana kuwa na tabia mbaya, mimba za utotoni kutokea,pia wengi wao hushawishika kuacha masomo pasipo kujua madhara yake".
Hivyo matumizi ya pombe kwa vijana wakiwa na umri mdogo huchangia vijan wengi kuporomoka kimaadili na wengine kushuka katika masomo kutokana na matumizi ya pombe wakiwa naumri mdogo, licha ya hvyo wazazi na walezi wanapaswa kuwalea watoto katika maadili bora.
