Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
HALI YA BIASHARA MSIMU WA MFUNGO

HALI YA BIASHARA MSIMU WA MFUNGO

  


NA EASTER KAMETA(UoI)

MATUKIO DAIMA

Baadhi ya wafanyabiashara wa  viungo vya chakula mkoani Iringa wameeleza juu ya hali ya biashara hisusani msimu huu wa mfungo wa kwaresma na ramadhani.

Wakizungumza na Matukio Daima Media  wafanyabiashara  wa viungo vya chakula  amedai kuwa kwasasa wateja wameongezeka kutokana na matumizi ya futari jioni huku akitaja baadhi ya viungo kama  pilipili , mdarasini ,iriki  kuwa ni muhimu katika futari.

"Mahitaji ya viungo yanaongezeka sana katika kipindi hiki ambacho watu wengi walio funga wanahitaji viungo hasa katika maandalizi  vyakula maalum wakati wa kufuturu  jioni matumizi ya viungo kamaVitunguu Tangawizi, Kitunguu swaumu ,Pilipili ,Mdalasini, karafuu,na iriki  uongezeka kwa sababu vyakula vya futari kama vile sambusa, supu, wali, nyama ."

Japhet Muhando ameeleza juu ya bei za viungo ambazo zimepanda kutokana na uhitaji wa watu pia ametaja kuwa bei hizi zimekuwa faida kwa wafanyabiashara wakubwa kwani inawapatia faida.

" Bei imepanda kutokana na ongezeko la uhitaji   wa  Vitunguu na tangawizi hivyo hufanya wafanyabiashara kupandisha   bei   hasa kipindi hiki cha mfungo  pia Wafanyabiashara wa jumla hupata wateja wengi Kutoka sehemu mbalimbali kama vile mahotelini, mama lishe, wauza futari hivyo hufanya wao kupata faida"

Vilevile Jenister Mlelwa amesema kuwa ushindani umeongezeka kutokana na kwamba baadhi ya wananchi wanapenda kufanya biashara za mda mfupi  ili kuweza kujipatia faida kubwa pia huku akutaja kuwa wengine hukosa faida kutokana na mitaji midogo.

"Ushindani unaongezeka kwa sababu watu wengi huingia katika biashara ya muda mfupi ili kuwezakupata faida kubwa hasa vijana ,Mama lishe, Wafanyabiashara wadogo hali hii  husababisha kushuka kwa faida kwa wafanyabiashara ambao ni wadogo pia kupoteza mitaji  yao kutoka na watu wengi kuuza bidhaa aina moja katika sehemu moja."


 shizya Mmbwaga  ameeleza juu ya utunzaji wa viungo vya chakula kuwa ni mgumu  hasa msimu huu wa mvua ,pia ametaja kuwa upatikanaji wake ni mgumu kwa baadhi ya viungo na kupelekea  wafanyabiashara wengi kuchukua bidhaa nyingi hadi  hupelekea kuadimika sokoni .


 "Utunzaji wa viungo vya chakula msimuu huu wa mvua ni mgumu pia upatikanaji mgumu  kwani baadhi ya bidhaa hupatikana kwa msimu hivyo hufanya wauzaji wengi hukimbilia kununua kwa wakati mmoja bidhaa ambapo hupelekea kuadimika  kwa  haraka sokoni ,hali hii hupelekea watu wenye mtaji mdogo   kukosa uhakika wa bidhaa  pia  biashara zao kuyumba"

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3