TANESCO KAGERA YAPOKEA VITENDEA KAZI VYENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.3
Na Anold Deogratias Matukio Daima Media
Shirika la umeme nchini TANESCO mkoa wa Kagera limepokea vyombo vya usafiri 29 vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.3, vitakavyosaidia kutoa huduma kwa wananchi na wateja washirika hilo kwa urahisi.
Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea vyombo hivyo meneja wa TANESCO mkoa wa Kagera Tawakal Seleman amesema kuwa vyombo hivyo vitakuwa msaada mkubwa katika kutoa huduma kwa wananchi na wateja wao kutokana na uhitaji mkubwa uliokuwepo kwa kuwa baadhi ya vyombo vya usafiri vilikuwa vimeharibika.
“vifaa hivi vitakuwa msaada mkubwa kwa shirika katika kuwahudumia wananchi tulikuwa na magari 59 kwa mkoa wa Kagera lakini magari 15 yameharibika hivyo kushindwa kutoa huduma kwa baadhi ya maeneo hivyo kupata vyombo hivi 29 itasaidia kufika hata maeneo ambayo yalikuwa hayafikiki”
Aidha Selaman amesema kuwa wanalengo la kufikia kaya laki 3 na eflu 15 kwa miaka mitano ijayo ambapo kila mwaka wanatarajia kufikia kaya efu 63 na 49 katika kutoa huduma kwao na pia kuwaunganishia umeme.
“lengo ni kufikia wateja elfu 63 na 49 kila mwaka ambapo kwa miaka mitano lengo ni kufikia kaya laki 3 na eflu 15 kwa hiyo tunategemea vyombo hivi vitatusaidia na kutimiza majukumu yetu na sisi tutafanya kazi zetu kwa juhudi na kujituma”
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Yahya Ramadhani Kido amelitaka shirika hilo kuvitunza vyombo hivyo kwa uangalifu mkubwa ili vidumu kwa muda mrefu na kwa huduma zilizolengwa kutolewa na serikali kwa wananchi.
“nitoe maelekezo kwa uongozi wa TANESCO mkoa wa Kagera kuhakikisha mnavitunza vifaa hivi ili vidumu na kutoa huduma zilizokusudiwa na serikali kwa wananchi na pia ni vyema zaidi mhakikishe magari haya wanapewa madereva ambao wanavigezo na uiijuzi wa kuendesha magari ya serikali”
Naye meneja wa TANESCO wilaya ya Kyerwa Hamza Halmas amesema kuwa usafiri ni nyenzo muhimu kwa shirika hilo katika kuwahudumia wananchi na wa wateja wao hivyo watavitumia vyema vifaa hivyo katika kuwahudumia wananchi wa wilaya ya Kyerwa kuhakikisha wanapata huduma bora.
“nyenzo muhimu katika kazi utendaji wetu wa kazi mojawapo ni usafiri kwa maana tumepata usafiri sasa tukutane saiti tunaenda kupambana katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora”
Miongoni mwa vifaa vilivyokabithiwa kwa shirikala hilo mkoa wa Kagera ni pamoja na magari aina ya Landcruser, Fuso yenye uzito wat ani 7 ikiwa na winchi yenye uwezo wa kunyanyua tani 3, pikipiki pamoja na bajaji.


.jpeg)

