Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MIGOGORO YA ARDHI INAKWAMISHA MIPANGO YA UCHUMI : DC CHUACHUA

MIGOGORO YA ARDHI INAKWAMISHA MIPANGO YA UCHUMI : DC CHUACHUA

 


Maafisa ardhi na  watendaji wa kata katika halmashauri ya wilaya Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji wakishughulikia maelekezo ya Mkuu wa wilaya Kigoma kushughulikia migogoro ya ardhi ya wananchi iliyoibuliwa kwenye Samia Ardhi Kliniki manispaa ya Kigoma Ujiji

Na Fadhili Abdallah,Matukio Daima Media Kigoma

MKUU wa wilaya Kigoma Dk.Rashid Chuachua amesema kuwa amepania kumaliza migogoro ya ardhi iliyopo katika halmashauri mbili za wilaya hiyo kwani migogoro hiyo ni sumu kubwa katika kuvutia wawekezaji.

Mkuu wa wilaya Kigoma Dk.Rashid Chuachua akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya Samia Ardhi Kliniki manispaa ya Kigoma Ujiji Machi 2 mjini Kigoma


Dk.Chuachua alisema hayo akizundua zoezi la wiki moja la kusikiliza kero za wananchi zinazohusu migogoro ya ardhi maarufu kama Samia Ardhi kliniki ikiwa kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake itakayofanyika Mach inane mwaka huu.


Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa anashangazwa kuona baadhi ya migogoro inachukua muda mrefu kupatiwa ufumbuzi ambapo migogoro mingine inarithiwa na hadi wajukuu jambo ambalo halina afya katika kushughulikia kero za wananchi hivyo ametaka wiki hii kutumika vizuri kumaliza migogoro ya muda mrefu ya ardhi kwenye wilaya hiyo.


Pamoja a hilo amewataka watendaji wa idara ya ardhi katika halmashauri za wilaya hiyo na maafisa watendaji kutimiza wajibu na majukumu yao kwa haki bila kumuonea mtu wala kushawishiwa na chochote na kwamba wakifanya hivyo migogoro mingi itapatiwa ufumbuzi huku akiwataka wananchi kutopandikiza migogoro kwa maslahi yao binafsi.


Baadhi ya wananchi waliohudhuria kliniki hiyo akiwemo Asha kavome kutoka manispaa ya Kigoma Ujiji alisema kuwa mgogoro wake umechukua muda mrefu kupatiwa ufumbuzi na amefika hadi ofisi ya  Mkuu wa mkoa na Kwa waziri wa Ardhi na suala hilo kurudisha idara ya ardhi ya manispaa Kigoma Ujiji lakini hadi leo hakuna ufumbuzi wowote uliopatikana.

Wakazi wa manispaa ya Kigoma Ujiji waliohudhuria Samia Ardhi Kliniki iliyozunduliwa uwanja wa Community Centre mjini Kigoma Machi 2  mwaka huu


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3