MAKAMU WA RAIS BALOZI NCHIMBI AZINDUA MFUMO WA KUTABIRI KIASI CHA MAJI KWENYE MITO
📌Azitaka taasisi za Serikali kujenga ushirikiano na sekta binafsi katika kukabiliana na changamoto ya maji
Na Lilian Kasenene, Morogoro
Matukio Daima Media
MAKAMU wa Rais Balozi Dk Emmanuel Nchimbi ameitaka wizara ya maji na taasisi zote za Serikali kujenga mtandao wa ushirikiano na sekta binafsi kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo huku akiwahimiza wadau wa maendeleo kulinda na kutunza vyanzo vya maji ili kwenda sambamba na dhamira ya rais ya kumtua mama ndoo kichwani.
Dk Nchimbi alisema hayo mjini Morogoro wakati wa maadhimisho kilele cha wiki ya maji kitaifa na siku ya maji Duniani.
Dk Nchimbi alisema kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya maji duniani, isemayo "maji na jinsia" imekuja wakati muafaka kwani wanawake wamekuwa waathirika wakubwa kiusalama kutokana na changamoto za maji ambapo asilimia tano ya hasara inayopatikana duniani, karibu dola bilioni 170 inatokana na kukosekana maji .
"Wanawake Wana mchango wa kipekeebama shida ama Raha katika maji ni zaidi ya asilimia 60 wamekuwa watu wa maji usiku na mchana katika changamoto ya na utunza familia,",alisema.
Alisema hadi sasa vijiji 10, 758 vimefikiwa na maji safi na salama ambapo bado vijiji 1575 havijafikiwa huku wizara hiyo imeshaweka mikakati ya kuvifikia
Makamu huyo wa Rais alisema kupitia sera ya maji ya mwaka 2022 Tanzania imepata mafanikio ambapo asilimia 92.5 ya Watanzania waishio mjini na asilimia 85.2 wanapata maji safi na salama .
Alisema katika Dira ya maendeleo ya Taifa 2050 inakadiriwa kuwa idadi ya watu itaongezeka hadi kufikia watu milioni 118 wengi wao wakiwa ni wa maeneo ya mijini ambapo itazalisha changamoto nyingi zikiwemo Elimu, chakula, Afya, Ajira na kubwa zaidi ni Maji.
"Ni muhimu kulinda na kutunza vyanzo vya maji, na uwekezaji uzingatie sera na dira ya maendeleo ya Taifa,"alisema.
Aifha alisema nia ya Serikali ni kuona mpango wa gridi ya maji ya Taifa inafanikiwa, sambamba na kufungwa kwa mita janja ili kumfanya mtumiaji awajibike na kuzuia upotevu wa maji.
Alisisitiza kubuni vyanzo vipya vya mapato badala ya kutegemea vilivyopo ili kukuza sekta ya maji na kuimarisha huduma za usafi wa mazingira ikiwemo kudhibiti mfumo wa maji taka usiingiliane na mfumo wa maji safi na kuleta madhara kwa watumiaji.
Kabla ya kuwahutubia wananchi katika viwanja vya mkwawa Leaf, mkoani hapa Makamu wa Rais alitembelea bwawa la Mindu linalotegemewa kama chanzo kikuu cha maji na zaidi ya asilimia 75 ya wananchi wa mji wa Morogoro ambapo amezindua mfumo wa utabiri wa kiasi cha maji kwenye mito Tanzania, pamoja na kupanda mti.
Awali mkurugenzi wa bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu Eibariki Mmasi alisema mfumo huo wa utabiri wa kiasi cha maji kwenye mito Tanzania utakuwa na uwezo kutabiri yatakayotokea kwenye mito hiyo ndani ya siku kumi hadi miezi mitatu na hivyo kurahisisha kuchukua hatua za haraka na uhakika kutokana na hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
Uzinduzi huo umefanyika katika la Bwawa la Mindu Mjini Morogoro ambako amejionea namna Wizara ya Maji inavyoshiriki katika utunzaji, ulinzi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji.
Mhandisi Mmasi alisema mfumo huo ni Moja ya jitihada za Wizara ya Maji kuhakikishia inaondoa changamoto za Sekta kwa kuwezesha upatikanani wa taarifa sahihi za kiwango cha Maji.
Alisema Bwawa hilo ni sehemu ya maeneo yatakayonufaika na changamoto hiyo kwani linapokea maji kutoka sehemu mbalimbali za nchi
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, aliahidi wizara yake kutokuwa kikwazo cha upatikanaji wa maji kwa wananchi na kwamba sasa hakuna mtendaji atakayekaa ofisini.
"Katika Suala la maji Rais anataka matokeo, wewe makamu wa Rais wewe na waziri mkuu mnataka matokeo, sisi viongozi wa wizara hatutawaangusha na tunaahidi kutokuwa kikwazo kwenu na kwa Watanzania"alisema.
Naye Mwakilishi wa sekta binafsi mhandisi Ngwisa Mpembe, alisema Sekta binafsi hiyo iko tayari kushirikiana na Serikali ambapo hadi sasa wamefanya uwekezaji wa zaidi ya shilingi Trilioni 1.2 kwenye sekta maji.
Alisema uwekezaji huo ni pamoja ujenzi wa viwanda vya mabomba ya maji, vifaa vya ujenzi vya maji, mita jinja na wamekusudia kuboresha zaidi katika teknolojia , Rasilimali watu na kutengeneza wztaalam wa ndani.
Aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuwekeza ,kufanya ubunifu , ujenzi wa miundombinu , teknolojia, usafi wa mazingira, kulinda vyanzo vya maji na upatikanaji wa fedha ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa maji kwa wote.
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Hassan Zungu alisema Bunge litahakikisha linaunga mkono masuala yote yanayopelekwa bungeni yanayohusiana na maji.
Alisema wizara ya Maji inaleta matumaini makubwa kwa Watanzania na kwamba hivi karibuni changamoto ya maji itaisha kutokana na hatua zinazochukuliwa na wizara hiyo.
Alimpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani kwa kutekeleza mradi wa bwawa la Kidunda lililopo mkoani Morogoro ambalo tangu mwaka 1954 lilianza kuzungumziwa.






.jpg)