lMAKAMU WA RAIS NCHIMBI MGENI RASMI KILELE WIKI YA MAJI MOROGORO
Na Matukio Daima, Morogoro
Macho na masikio ya wadau wa maendeleo yameelekezwa mkoani Morogoro, ambako Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Wiki ya Maji ambayo Kitaifa kwa mwaka 2026 yanafanyika Mjini Morogoro.
Tukio hilo kubwa litakalofanyika katika viwanja vya Mkwawa Tobacco Leaf, linatarajiwa kukutanisha viongozi wa Serikali, Wabunge, wataalamu wa sekta ya maji pamoja na wananchi, likiwa na ajenda kuu ya kujadili maendeleo na changamoto za upatikanaji wa maji nchini.
Mbali na hotuba ya mgeni rasmi, ratiba inaonesha uwepo wa uzinduzi wa miradi ya Maji, upandaji miti kuzunguka Bwawa la Mindu, maonesho na mijadala ya kitaalamu, yote yakilenga kuunga mkono kaulimbiu ya mwaka huu: “Maji na Jinsia”.
Mwisho
