ISRAEL YASHAMBULIA 'MAKAO MAKUU YA USALAMA' MJINI TEHRAN
Moshi ukifuka juu ya Tehran
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema kuwa Iimeshambulia makumi ya shabaha za kijeshi kote mjini Tehran, Msemaji wa Jeshi hilo Avichay Adraee ametangaza.
Mashambulizi hayo yalilenga makao makuu ya Basij - kikosi cha kijeshi chenye uhusiano na Walinzi wa Mapinduzi wa Iran - Ikiwa ni pamoja na zana za kurushia makombora na mifumo ya ulinzi, pamoja na "kurugenzi ya ugavi na usafirishaji inayoshirikiana na vikosi vya ardhini vya serikali".
Anaongeza kuwa IDF itaendelea "kuongeza mashambulizi yake" dhidi miundombinu ya serikali ya Iran.
Kambi ya Al Udaid yashambuliwa
Wakati huo huo Qatar imeshambuliwa kwa makombora mawili ya masafa marefu, Wizara yake ya Ulinzi inasema.
Moja kati ya makombora hayo ilizuiliwa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Qatar, huku moja ikigonga kambi ya Al Udaid -kambi kubwa ya jeshi la anga la Marekani katika eneo hilo.
Qatar inasema hakuna majeruhi waliyoripotiwa katika shambulio hilo.